Wahandisi wapata matumaini mapya ya kujiimarisha katika miradi ya serikali

 

Matumaini yajazwa katika Kilele cha Mkutano wa  21 Wahandisi kwa kujadili vikwanzo ambavyo kwao vilionekana vinakwamisha utendaji wao.

Katika Mkutano wamejadili mada mbalimbali ikiwemo fursa za Wahandisi wa Wazawa katika miradi ya Serikali ambapo walikadili namna bora ya kuiendea miradi hiyo kwa mustakabali bora wa fani ya uhandisi nchini.

Mkutano huo wa 21 umetanguliwa na mikutano mingine ikiwa pamoja na kulea Wahandisi vijana katika kushiriki pamoja na kuanzisha kampuni nao waweze kupata manufaa yao binafsi  lakini taifa kuweza kupata maendeleo kutokana na mchango wao.

Akizungumza katika Kilele cha Mkutano wa 21  wa Wahandisi  uliofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam Waziri Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Mapinduzi Zanzibar Rahma Kassim  Ali amesema dhamira ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza, kuilinda, na kuendeleza fani ya Uhandisi nchini.

Amesema kuwa  majadiliano katika mkutano unaonyesha mwanga  kutokana na kupata mawazo na ndoto za wahandisi vijana, wazee, na wadau mbalimbali wanaoshirikiana kukuza sekta muhimu ya Uhandisi.

Hata hivyo aliweka  wazi kwamba uhandisi ni uti wa mgongo wa maendeleo ya taifa, hususan katika nyanja za mapinduzi ya kiteknolojia ya ujenzi wa kisasa unaokwenda kupendezesha nchi na kupata maendeleo yanayotokana na Teknolojia hizo.

 Rahma  aliwahimiza wahandisi kuunga mkono mpango wa mradi wa STEAM, mradi wenye malengo ya kuhamasisha vijana kujiunga na sekta ya uhandisi kwa vitendo.

“Tunawahitaji vijana katika uwanja huu, kwa sababu wao ndiyo watakaosukuma mbele teknolojia za kesho tofauti na sasa jinsi tulivyo “amesema Waziri Rahma Kassim Ali.

Waziri Rahma amesema vijana Wahandisi wanatakiwa kuandaliwa wakiwa na Ubunifu na uthubutu wa kufanya kazi ya Uhandisi kuendelea kuleta maendeleo.

Msajili wa Bodi ya Wahandisi Tanzania (ERB),Mhandisi Bernard Kavishe amesema kuwa  bodi yake katika kukuza taaluma ya uhandisi  imejizatiti kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wahandisi wanapata mazingira bora ya kufanya kazi na kuboresha ujuzi wao.

Amesema katika mipago mikakati ya bodi ni kuhakikisha Wahandisi nchini wanakuwa suluhisho katika changamoto zinazoikabili nchi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education, AbdulMalik Mollel amesema Taasisi yake ipo tayari kushirikiana na Bodi ya Wahandisi Tanzania ili kutoa fursa za elimu na ujuzi bora katika vyuo vya nje ya nchi itakayowasaidia wahandisi vijana kuwa na maarifa sahihi katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia. 

“Tunaamini kwamba kwa kutoa elimu bora, tutawawezesha wahandisi wetu kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa,” amesema Mollel 

Naye Dkt. Kisenge, Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), aliweka msisitizo kuhusu mchango wa wahandisi katika sekta ya afya, hasa kwenye maendeleo ya vifaa tiba na miundombinu ya kisasa inayosaidia kuboresha huduma za afya nchini. Aliahidi kushirikiana na bodi hiyo kwa karibu ili kuhakikisha fani ya uhandisi inazidi kukua.

Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe akitoa maelezo kuhusiana na umuhimu wa mkutano kwa Wahandisi uliofanyika na kufungwa katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya matukio katika picha wakati wa ufungaji wa mkutano wa 21 Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Related Posts