Na Chedaiwe Msuya,WF
Wizara ya Fedha imehitimisha utoaji wa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi kwa Umma katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara ili yakilenga kuwapa uelewa kuhusu Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Sura namba 410.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPPC), Bi. Flora Tenga alisema kuwa malengo ya mafunzo yalikuwa kuwaelimisha maofisa mipango na viongozi wote wanaohusika na ununuzi ili kufahamu fursa zilizopo katika Sheria hiyo na namna wanavyokwenda kuitekeleza.
“Sheria ya Ubia kati Dekta ya Umma na Sekta Binafsi imetoa fursa mbalimbali katika miradi ya ubia ambapo kuna fursa na vivutio vingi vinavowavutia wawekezaji huku lengo lingine ni kuhusu Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura Na. 103 iliyofanyiwa marekebisho mbalimbali na kutoa fusa mbalimbali katika miradi ya ubia,” alisema Bi. Flora
Lifafanua kuwa kuna fursa nyingi, kuna vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi ambavyo vinavutia wawekezaji na kuna vivutio mbalimbali ambavyo wanataka kuwaelimisha wanaotekeleza miradi ya ubia.
Pia amewataka wanaotekeleza miradi ya maendeleo, badala ya kusubiri fedha za Serikali kutekeleza miradi hiyo watumie Sheria hiyo kumwalika mbia mwekezaji aweze kuleta fedha za kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo ikiwemo miradi midogo midogo inayotekelezwa kwenye Serikali za Mitaa
Vilevile alisema kuna Sheria ya Takwimu kwani maendeleo au mipango yoyote haiwezi kupatikana bila kujua takwimu zilizopo.
“Kwahiyo tuko hapa pia kuwaelimisha Maafisa Mipango na viongozi wengine namna ya kutumia Takwimu sahihi”alisema Bi. Flora
Naye Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kusini, Fenias Manasseh alisema kuwa wamelazimika kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa Serikali kutoka sekta mbalimbali ili kuwapatia elimu hiyo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ili waweze kujua fursa na mabadiliko yaliyopo kwenye Sheria hiyo ili waweze kufaidika nazo.
“Wengi wao hapa wanataka katika Taasisi Nunuzi wanaofanya kazi ya michakato ya ununuzi sasa kama hawaelewi mabadiliko yaliyojitokeza kwenye Sheria ya Ununuzi wa Umma wataendelea kuwa na mambo ya kizamani na kusababisha wahusika washindwe kufaidi hizi fursa nyingi mbalimbali za maendeleo,”alisema Bw. Manasseh.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdillah Mfinanga alisema kuwa Wizara hiyo inaendesha mafunzo kwa watendaji wa Serikali waliopo katika ngazi za mikoa, halmashauri, majiji, miji na wilaya kufuatia kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazohusu utekelezaji wa Sheria hiyo.
Aidha mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ni pomoja na utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma lenye lengo la kuwafahamisha watanzania juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika sheria hiyo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Abdilai Mfinanga, akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mtwara, Lindi na Ruvuma kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Mtwara
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Bi. Flora Tenga, akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mtwara, Lindi na Ruvuma kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Mtwara
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kusini, Fenias Manasseh akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mtwara, Lindi na Ruvuma kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Mtwara
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mtwara, Lindi na Ruvuma na watumishi wa Wizara ya Fedha wakiwa kwenye mafunzo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Mtwara
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF – Dodoma)