Baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Bagamoyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliowasili kutoa elimu ya fedha kwa watumishi, kuhusu usimamizi wa fedha binafsi, dhamana za mikopo, riba pamoja na uwekezaji, katika ukumbi wa mikutano wa wilaya ya Bagamoyo, Pwani.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha Bw. Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa wanapochukua mikopo ili kuwawezesha kuondokana na mikopo umiza pamoja na umuhimu wa kuzingatia mapato na matumizi ili wajiwekee akiba, wakati Maafisa wa Wizara ya Fedha walipokuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (TaSUBa), Bagamoyo, Pwani.
Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akifafanua jambo kwa wananchi mara baada ya kukamilika kwa programu ya elimu ya fedha kwa wananchi inayotekelezwa na Wizara ya Fedha, iliyofanyika katika wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (TaSUBa), Bagamoyo, Pwani.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Bagamoyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliowasili kutoa elimu ya fedha kwa watumishi, kuhusiana na usimamizi wa fedha binafsi, dhamana za mikopo, riba pamoja na uwekezaji, katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (TaSUBa), Bagamoyo, mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Bagamoyo wakisoma vipeperushi walivyopewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliowasili kutoa elimu ya fedha kwa watumishi, kuhusiana na usimamizi wa fedha binafsi, dhamana za mikopo, riba pamoja na uwekezaji, katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (TaSUBa), Bagamoyo, Pwani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Bagamoyo -Pwani)