Dar es Salaam. Katika kukuza idadi ya wanawake katika nafasi za maamuzi, Benki ya Stanbic imetaja mradi wake wa ‘kuwasha’ kuwa chachu katika kuibua talanta za uongozi kwa jinsia hiyo.
Ujumuishi wa wanawake katika nafasi hizo hasa katika sekta ya fedha unatajwa kuongeza ubunifu na maamuzi sahihi.
“Uongozi unaozingatia ujumuishi wa jinsia, huboresha ubunifu na maamuzi, na pia huwa stahimilivu,”Hii ni kwa muujibu wa majarida ya Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na kurejelewa na muongozo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa mabenki na taasisi za fedha wa tarehe 22 Agosti 2024.
Mkuu wa Idara ya Watu na Utamaduni wa Stanbic Bank Tanzania, Rabina Masanja, amesema lengo la hatua hiyo ni kufikia uongozi jumuishi kijinsia.
“Stanbic Bank Tanzania, tunaamini kwamba mustakabali wa benki yetu unategemea juhudi za kimkakati tunazochukua leo kuibua vipaji vya viongozi wetu wa kike. Mpango huu wa “Ignite” au ‘kuwasha’ ni zaidi ya mafunzo. Mpango huu unawajengea wafanyakazi wanawake uwezo wa kuongoza na kujiamini, na hatimaye kuwafungulia fursa za kuongoza.,”amesema Rabina.
Rabina ameongeza kuwa; “Mwaka huu, Stanbic Bank tumezindua awamu ya tatu ya mpango wa “ignite”, zikiwa juhudi za kuwawezesha wanawake wengi zaidi kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za uongozi. Kwa namna ya kipekee, Stanbic Bank pia imezingua mpango wa “Re-Ignite”, yaani kuwasha tena, ikilenga wahitimu wa awamu zilizopita, ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa na mikakati endelevu ya uongozi.
Naye, Violet Moirdichai, mjumbe wa wa Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Stanbic “Uongozi ni safari, sio marudio. Kupitia mpango wa “Re-Ignite”, tunahakikisha kwamba wahitimu wetu wanaendelea kukua na kuongoza kwa ubora.”