MZEE BUTIKU AITAKA TAIFA KUPIGA VIKALI TABIA MBAYA ZA KULAWITI NA KUNYANYASA WATANZANIA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana kwa umoja katika kupinga tabia mbaya zinazozidi kuibuka nchini, ikiwemo kulawiti, kuteka, kunyanyasa, na kuua watu. Akizungumza mbele ya wanahabari leo, Jumanne tarehe 10 Septemba 2024, jijini Dar es Salaam, Mzee Butiku amesisitiza umuhimu wa umoja katika kukabiliana na matukio haya.

” ndugu wanahabari, tumewaiteni hapa (kwenye Ofisi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere) kuwataarifu Watanzania wote na kuwaomba kwamba sisi sote tushirikiane kuunga mkono katika kupinga tabia mbaya zilizozuka katika Taifa letu za kulawiti, kuteka, kunyanyasa, na kuuwa Watanzania wenzetu,” amesema Mzee Butiku.

Ameeleza kuwa tabia hizi zinachafua jina la nchi na kuleta madhara makubwa kwa jamii, hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua hatua na kuwa sehemu ya mapambano dhidi ya ukatili huu. Mzee Butiku aliongeza kuwa Taasisi ya Mwalimu Nyerere itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa jamii inapata ulinzi na haki inatendeka kwa wote.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts