RISASI na Kahama Sixers zimeianza vizuri kampeni ya kuwania ubingwa wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Shinyanga baada ya kushinda katika hatua ya kwanza ya nusu fainali.
Katika mchezo wa kwanza Risasi iliishinda Veta kwa pointi 12-80, huku Kahama Sixers ikifunga B4 Mwadui kwa pointi 80-75.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kamishina wa Ufundi na Mashindano wa mkoa huo, George Simba alisema nusu fainali itachezwa mara tatu kwa mfumo wa ‘best of three play off.’
“Timu itakayoshinda mara mbili mfululizo itakuwa imeingia fainali kwa kushinda michezo 2-0,” alisema Simba.