Mikumi safi majaribio timu ya taifa kriketi

TIMU ya Mikumi imepata ushindi wa tatu dhidi ya Ngorongoro katika kriketi, ambapo safari hii imeshinda kwa wiketi mbili kwenye Uwanja wa Dar Gymkhana.

Timu hizo za kombani zinaundwa na wachezaji nyota wa kriketi nchini kama maandalizi ya timu ya taifa kwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia zitakazochezwa Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi huu.

Wachezaji ambao wanaunda Mikumi na Ngorongoro wamekwisha- cheza mara nne na Mikumi kushinda tatu wakati Ngorongoro ikishida moja.

Ngorongoro ndiyo walioanza kubeti na kufanikiwa kutandaza mikimbio 153 baada ya kumaliza mizunguko e 20 na kupoteza wiketi 6.

Mikumi  walitengeneza mikimbio 155 huku wakiangusha wiketi 8 baada ya kutumia mizunguko  19.

Licha ya kufungwa, Alishihab Bukhari wa Ngorongoro aliongoza kwa mikimbio baada kutengeneza 66 peke yake. Wakati huohuo, Annadil Burhan imenyakua ubingwa wa kriketi wa Dar es Salaam kwa mizunguko 30 kwa kuifunga Caravans katika Uwanja wa Annadil Burhan. 

Caravans ndiyo walioanza kubeti na kutengeneza mikimbio 56 baada ya wote 10 kutolewa wakiwa wametumia mizunguko 14 kati ya 30 iliyowekwa.

Haikuwa  tabu kwa Annadi Burhan kuzifikia alama hizo, kwani iliwachukua  mizunguko 14 kati ya 30  kutengeneza mikimbio 58  huku ikipoteza wiketi mbili.

Annadil Burhani wametawazwa mabingwa wa mizunguko 30 kwa ushindi wa wiketi 8. Hatim Dahodwala alikuwa shujaa kwa washindi baada kuangusha wiketi 5 za wapinzani peke yake akifuatiwa na Alfred Daniel wiketi 2.

Katika hatua nyingine, Lions C imetinga fainali ya Kombe la TCA kwa division C baada ya kuitoa MCC kwa mikimbio 10. Lions C ndiyo walioanza kubeti na kutengeneza  mikimbio  147 huku wakiangusha wiketi 7 baada ya kumaliza mizunguko 20.

Related Posts