WAZIRI JAFO: ONGEZENI KASI YA UZALISHAJI SUKARI

Waziri wa viwanda na biashara Dkt. Selemani jafo (Mb) akipokea maelezo ya jinsi mtambo wa kisasa wa kupakia sukari unavyofanya kazi pamoja na mchakato mzima wa uzalishaji sukari unavyofanyika kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa Group Bw Hussein Sufiani alipotembelea kiwanda hicho Septemba 11, 2024

……

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo (Mb) amekishauri Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kuongeza kasi ya uzalishaji wa sukari
ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa sukari hasa katika kipindi cha mvua ambapo viwanda vingi husimamisha zoezi la uzalishaji kutokana na athari za mvua .

Dkt Jafo ameyasema hayo Septemba 11, 2024 alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kilichopo kilichopo Makurunge Bagamoyo Mkoani wa Pwani kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza na kitatua changamoto zao

Katika ziara hiyo Waziri Jafo aliushauri uongozi wa Kiwanda hicho kuongeza bidii kwenye uzalishaji wa sukari nchini katika ambapo kwa sasa

“Nchi yetu mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 802000 ambayo inajumuisha industrial sugar (sukari ya viwandani) tani 250000, na ile ( brown sugar )sukari ya nyumbani ambayo tunatumia kwa kunywa ni tani 552000 hivyo nimefurahia uwekezaji huu.” Alibainisha Dkt Jafo.

Aidha, Dkt Jafo amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya sukari nchini kuwa Serikali itaendela kuwalinda na kuwatengenezea mazingira wezeshi ya uwekezaji.

“Rais Samia dhamira yake kubwa ni kuvilinda hivi viwanda kwa nguvu yote na mimi hili jimbo la viwanda ni jimbo langu nina majimbo mawili jimbo la Kisarawe na jimbo la viwanda.”

Aidha Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Bw. frank Nyabundege ametoa msisitizo kwa wazalishaji wa sukari nchini kutosita pale wanapohitaji msaada kutoka katika benki hiyo.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa Group Bw Hussein Sufiani amesema kiwanda hicho kinauwezo wa kuzalisha wastani wa tani 1800 hadi 2000 kwa siku na jumla ya wastani wa tani 80000 zinatarajiwa kuzalishwa na kiwanda hicho malengo yakiwa ni kufikia tani 100000.

Aidha, kiwanda hicho kinatoa ajira ajira zaidi ya 1500 kwa awamu ya kwanza na kikikamilika awamu zote tatu kitatoa ajira zaidi ya 3000 na
Kitakuwa na Mtambo wa kufua umeme wa Megawati 5 utakaokuwa
unatumia taka zinzotoka kiwandani kuzalisha umeme.

Waziri wa viwanda na biashara Dkt. Selemani jafo (Mb) akipokea muhtasari wa kuanzishwa kwa Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo Sugar kilichopo Makurunge, Bagamoyo Pwani wenye wastani ya kilometa za mraba elfu 10 kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa Group Bw Hussein Sufiani alipotembelea kiwanda hicho.

Waziri wa viwanda na biashara Dkt. Selemani jafo (Mb) akipokea maelezo ya jinsi mtambo wa kisasa wa kupakia sukari unavyofanya kazi pamoja na mchakato mzima wa uzalishaji sukari unavyofanyika kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa Group Bw Hussein Sufiani alipotembelea kiwanda hicho Septemba 11, 2024

Related Posts