Raia wa kigeni waangukia mikononi mwa Polisi wadaiwa kutaka kumuibia mfanyabiashara aliyetoka benk

Watu wawili ambao ni raia wa kigeni wamekamatwa na Polisi mkoani Njombe kwa tuhuma ya kutaka kumuibia Mtanzania aliyekuwa akitoka benki mjini Makambako.

Akizungumza na vyombo vya habari Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Ally Kitumbu amesema Raia hao wa kigeni wamefahamika kwa majina ya Ommary Keny (40) pamoja na Hamphrey Jailo (22) bila kutaja nchi zao waliweza kuwakamata baada ya kupata taarifa za watu hao wakimfuatilia mfanyabiashara aliyetoka benki.

Amesema kwa mujibu wa taarifa walizonazo ni kuwa watu hao wamekuwa wakijihusha na wizi katika maeneo mbalimbali nchini ambapo hutumia funguo zao bandia kufungua magari wanapobaini uwepo wa fedha kwenye gari ya mtu iliyopaki.

“Wana kawaida ya kukaa kwenye maeneo ya mabenki wakiangalia nani anatoka na begi wakiamini begi hilo lina fedha sasa ukiweka kwenye gari wanakufuatilia na ukipaki gari na kutoka wao huwa wanakuwa naa master Key,wanafungua wanachukua fedha na gari lako wanalifunga”amesema Kitumbu

Kitumbu amesema wakati wakikamatwa mjini Makambako kuna mtu mmoja alitoka benki ya NMB na kuanza kufuatiliwa alipoingia kwenye gari yake lakini wananchi walitia mashaka na kumpa taarifa anayefuatiliwa juu ya uwepo wa gari nyuma inayomfuatilia ndipo mfanyabiashara huyo alifanikiwa kutoa taarifa kituo cha Polisi na askari wakaanza kufuatilia mpaka wakaweza kuwakamata.

Related Posts