Mnamo Mwezi Aprili na Oktoba, 2023 katika nyakati tofauti huko Kijiji cha Nyanjati wilaya Kibiti Mkoa wa Kipolisi Rufiji.
Mshtakiwa Dadi Hamis Msumi (20) Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Nyanjati alimbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la Nne mwenye umri wa miaka 12 (Jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu ya kimwili na kisaikolojia.
Septemba 11,2024 baada ya shauri kusikilizwa mpaka mwisho kwa upande wa Mashtaka kuwaleta mahakamani mashahidi 07 akiwemo Mganga Mfawidhi Hospitali ya wilaya Kondoa, Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kondoa pamoja na ushahidi wa nyaraka 2, Shtaka lenye makosa mawili ya KUBAKA na KULAWITI lilithibitishwa pasi kuacha shaka na Mshitakiwa alikutwa na hatia na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha 30 jela kwa kosa la kwanza na kifungo cha miaka 30 kwa kosa la pili. Adhabu zote kwenda kwa pamoja.
Aidha Mahakama imemuamuru Mshtakiwa kumlipa muhanga fidia ya Shilingi milioni moja (1,000,000/=) kwa madhara aliyomsababishia.
Hukumu imesomwa mbele ya Mhe. Hakimu Tarsila John Kisoka – PRM II
#KonceptTvUpdates