HESLB na TRA zaungana kusaka wadaiwa mikopo Elimu ya juu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa Septemba 12, 2024) imebadilishana Hati za Makubaliano na taasisi ya kimkakati ambayo utekelezaji wake unalenga kubadilishana taarifa ili kuwasaka wadaiwa wa mikopo ya Elimu ya juu.

Taasisi hiyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Hafla ya kubadilishana hati hizo imefanyika katika ofisi za HESLB jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na watendaji wakuu wa taasisi hizo.

Akiongea katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia amesema lengo la ushirikiano na taasisi hiyo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni kuboresha huduma za Heslb na kuwafikia wadau mbalimbali nchini nzima.

‘Kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) tunaweza kutambua changamoto mbalimbali na hivyo sisi tukaboresha huduma zetu kwa mfano kwenye Mikopo tunayoitoa, huduma tunazozitoa tunaweza tukaboresha kupitia mabadilishano ya Kanzidata kati ya taasisi hizi mbili’

‘Vilevile hati hizi za ushirikiano zijatusaidia katika kuboresha huduma zetu badala ya Mwanafunzi kuwa anatumia muda mwingi kujaza fomu yake baadhi ya taarifa tunaweza tukazipata kwenye taasisi mbalimbali za Kiserikali ikiwemo TRA’

‘Jambo Hili litaendana na agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo aliagiza taasisi za Kiserikali mifumo yake yote isomane kabla ya Desemba Melaka 2024 na niseme kupitia Vyombo vyenu vya Habari kwamba hilo kushirikiana na TRA tutalikamilisha kikamilifu kabla ya kufika Desemba Maka 2024’ amesema Dkt. Kiwia.

 

’Baada ya kubadilishana hati hizi za ushirikiano litakalofuata ni vikao vya mkakati vya tathmini ambapo katika kikao cha tathmini tutaangalia jinsi gani taasisi hizi mbili zitatekeleza maazimio hayo’- amesema Dkt. Kiwia.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Yusuph Mwenda ameshukuru kwa taasisi yake kushirikishwa na kutoa wito kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha ili kujijengea uaminifu wa kukopesheka na taasisi za fedha.

‘Nawasihi wanufaika wa mikopo warejeshe sababu wao walipewa mikopo, kwakuwa kuna wengine walikopeshwa na wakarejesha’- amesema Yusuph Mwenda

Related Posts