UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA SASA NI ZAMU YA DODOMA NA SINGIDA

 

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani Dodoma leo Septemba 13, 2024. 

Mjumbe
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari
akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Singida leo
Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau
mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba
mosi mwaka huu.

Mjumbe
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari
akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Singida leo
Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau
mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba
mosi mwaka huu.

Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani
akiwasilisha mada ya Uboreshaji wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi
Mkoani Singida leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia
Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu. 

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Selemani Mtibora akiwasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,  mada ya Uboreshaji wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Dodoma leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu.


Wadau
wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu
wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki
katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024
mkoani Dodoma. 

Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024 mkoani Dodoma. 

Wazee wa kimila ni wadau muhimu wa uchaguzi
kutokana  na umri, hekima na busara zao. Tume
imekuwa ikishirikiana na wazee wa kimila katika kuwaelimisha na kuwashawishi
wananchi kujitokeza na kushiriki kwenye michakato ya uchaguzi. Pichani ni Chifu wa Mkoa wa Singida,
Mushenyi Senge Ndovu (kushoto) na Chifu wa Singida Vijijini, Kilongo Kika
wakiwa katika mkutano wa wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la
Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Septemba 13,2024 mkoani Singida. 

Wadau
wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu
wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki
katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024
mkoani Singida. 

***************

Na. Mwandishi Wetu

Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Singida, sehemu ya mkoa wa Dodoma na sehemu ya
mkoa wa Manyara utaanza tarehe 25 Septemba, 2024 hadi tarehe 01 Oktoba, 2024.


Makamu Mwenyekiti wa Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mstaafu, Mbarouk
Salim Mbarouk ameyasema hayo leo tarehe 13 Septemba, 2024 jijini Dodoma wakati
akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya zoezi hilo.


“Mzunguko wa tano wa
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utajumuisha mkoa huu wa Dodoma
katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri za Wilaya ya Bahi, Chamwino
na Kongwa, mkoa wa Manyara katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Wilaya ya
Kiteto na Simanjoro na mkoa wa Singida ambapo uboreshaji utaanza tarehe 25
Septemba, 2024 hadi tarehe 01 Oktoba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa
kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema.


Amefafanua kuwa uboreshaji
wa Daftari utahusu kuwaandikisha raia wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka
kumi na nane na zaidi au watakaotimiza umri huo wakati au kabla ya tarehe ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na ambao hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya
uchaguzi au sheria nyingine yeyote.


Katika hautua nyingine,
akifungua mkutano wa wadau mkoani Singida, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari amesema kuwa Tume
katika kuhakikisha kwamba inaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni
pamoja na kurahisisha zoezi hili la uboreshaji wa Daftari, imeboresha mfumo wa
uandikishaji ambao kwa mara ya kwanza utamuwezesha mpiga kura aliyepo kwenye
Daftari kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zake au kuhama kituo kwa
kutumia aina zote za simu au kompyuta.


“Wanaotumia simu za kawaida
(maarufu kama kitochi au kiswaswadu) nao wanaweza kutumia huduma hii kwa kupiga
namba *152*00# na kisha watabonyeza namba 9 halafu wataendelea na hatua zingine
kama itakavyokuwa inaelekezwa kwenye simu husika,” amesema.


Jaji. Asina amefafanua kuwa
mtumiaji wa huduma hii, atatakiwa kufika kituo anachokusudia kujiandikisha ili
akamilishe hatua za kupigwa picha, kuweka saini na kupatiwa kadi yake ya mpiga
kura.


Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulizinduliwa mkoani Kigoma
tarehe 20 Julai, 2024
sambamba na kuanza kwa
uboreshaji kwenye mikoa mitatu ya Kigoma, Tabora na Katavi na kufuatiwa na
mikoa ya Geit, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu na Manyara katika
Halmashauri za Wilaya ya Babati, Hanang, Mbulu na Mji wa Babati.


Kwa mujibu wa ratiba
iliyotolewa na Tume awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari inatarajiwa
kukamilika mwezi Machi, 2025.

Related Posts