VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA MSIINGILIE MCHAKATO WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA – JAJI MSTAAFU MBAROUK

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Mahakama ya Rufaa Mbarouk Salim Mbarouk amewasisitiza mawakala na viongozi wa vyana vya siasa kutokuingilia mchakato wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kituoni.

Jaji Mstaafu Mbarouk ameyasema hayo leo Septemba 13,2024 Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

“Hivyo niwaombe viongozi wa vyama vya siasa ba wadau wa uchaguzi kwa ujumla kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo ya Tume na kusimamia miiko na mipaka ya undeshaji wa zoezi la uboreshaji daftari,” amesem.

Aidha, ameongeza kuwa ni vyema wakatumia sheria zilizopo kuwasilisha kwa Tume changamoto zitakazijitokeza, na kuongeza kuwa kwa upande wao watazingatia katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi hilo la uboreshaji.

Pia amewahimiza wadau hao kupitia majukwaa kwenye majukwaa yao ya kisiasa, kijamii, kitamaduni, kiimani na kiuchumi kuwakumbusha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandilisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

“Ni mategemeo yetu kuwa michango na maoni watakayotoa kwenye mkutano huo yatakuwa na manufaa makubwa katika kutekeleza zoezi ambalo lipo mbele yetu,”ameongeza.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Selemani Mtibora amesema kwa mkoa wa Dodoma kuna vituo 2,721 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa nwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 37 katika vituo 2,684 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

Mtibora ameongeza kuwa jumla ya wapiga kura 594,494 wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo ambapo watakao kosa sifa wataondolewa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

“Hivyo, baada ya uboreshaji inatarajiwa kuwa daftari litakuwa na jumla ya wapiga kura 34,746,638 pia idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwq inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa daftari la uboreshaji mwaka 2019/20 lakini kwasababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha kuwa wapiga kura,” amesema.

Naye Mratibu wa uandikishaji Mkoa wa Dodoma Charles Mduma amevielekeza vyama vya siasa kuzingatia mafunzo na maelekezo yanayotolewa na tume yanl uchaguzi ili kila mtu atimize wajibu wake.

“Mafunzo haya ya leo tumepewa majukumu ya kwamba wanasiasa wanajukumu ganj katika zoezi hili la uboreshaji kwahiyo sana sana naendelea kuwaelekeza wafuate na kuzingatia yale yaliyofundishwa ili uchaguzi uweze kwenda vizuri,”amesema.

Related Posts