WANANCHI WATAKIWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZINAZOFANYWA NA THBUB

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi, akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa basi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), itakalowasaidia watumishi wake katika utoaji wa huduma kwa wananchi hafla uliofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa THBUB Jaji mstaafu Mathew Mwaimu,akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa basi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), itakalowasaidia watumishi wake katika utoaji wa huduma kwa wananchi hafla uliofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma

Na. Nuru Mangi, DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi amewataka wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), kwa kutoa taarifa zilizo sahihi ili kusaidia  katika chunguzi zinazofanywa na tume hiyo na kurahisisha ufanyaji kazi.

Maswi ameyasema hayo leo Septemba 13,2024 Jijini Dodoma katika hafla fupi ya uzinduzi wa basi la THBUB litakalowasaidia watumishi wake katika utoaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza kuwa ni muhimu serikali  kusimamia vyema haki za binadamu na kuangalia shughuli za wananchi.

“Tume yetu inafanya kazi kwa mujibu wa taratibu zetu zilizowekwa na kwa muujibu wa katiba hivyo tukio lolote linalotokea, tume ina haki ya kwenda na kufanya uchunguzi, hivyo tunachoomba kwenu nyie wana habari na watanzania wote kuunga mkono tume na kuwapa taarifa ili waweze kufanya kazi kulingana na sheria zilizopo kwa sasa,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa THBUB Jaji mstaafu Mathew Mwaimu ameomba wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwani jambo hilo siyo la kistaarabu huku akisistiza kuwa Tanzania ni nchi ya kistaarabu hivyo ustaarabu huo unataka wananchi wawe wanafanya kila jambo kwa kuzingatia utawala wa sheria.

“Si jambo jema sana kufikiria kwamba kila mtu anaweza kuondoa uhai wa mtu binafsi bila kufuata utaratibu wa kisheria.”

Sambamba na hayo Jaji Mwaimu amesema viongozi wote katika ngazi zote wanapaswa kujishugulisha katika kutoa elimu ili watu watambue umuhimu wa maisha ya binadamu.

Related Posts