Zimamoto sasa wageukia shuleni na hospitali elimu ya majanga

Katika kukabiliana na changamoto ya Majanga ambayo yanatokea kwenye jamii mbalimbali Jeshi la zimamoto a uokoaji wameendelea kutoa elimu Kwa makundi mbalimbali mkoani Morogoro

Akizungumza na wazazi pamoja na walezi mbalimbali Msemaji Mkuu wa jeshi la zimamoto n uokoaji nchini Naiibu kamishina Puyo Nzalayaimisi amesema kuwa asilimia kubwa ya matukio ya moto, kwenye majengo husababishwa na watoto

Aidha amesema kuwa kupungua kwa Malezi kwa watoto kunatajwa kuwa miongoni mwa sababu ambazo zimawafanya wazazi kuwaacha watoto peke yao na Wadada wa kazi mwisho wa siku kusababisha matatizo.

Amesema mpango wa jeshi hilo ni kuendelea kutoa elimu Kwa makundi mbalimbali ambapo mara hii wanafika kituo cha Afya mafiga na shuleni ambapo ameleza kuwa wazazi wawe makini na watoto kwani ndio wahanga wakubwa wa matukio ya moto wa nyumbani.

Kwa Upande wake Patricia Antony afisa Muuguzi amesema kuwa wamekuwa wakipokea watoto wakiwa na matatizo mbalimbali ambayo yanasababishwa na uzembe wa wazazi kuwaacha watoto peke yao na kuwataka wazazi kukaa na watoto wao

Amina Juma ni Miongoni mwa wazazi waliohudhuria katika elimu hii inayotolewa na msemaji mkuu wa wa jeshi la zimamoto na uokoaji wamesema kuwa imewapa mwanga na kuomba iwe endelevu na kuwafikia watu wengi kwani watu wanahitaji elimu

Amina ameliahukuru jeshi hilo Kwa elimu hiyo na kwamba jamii inatakiwa kurudi kwenye malezi ya watoto pamoja na kuwakumbusha wadada wa kazi naoma ya kuepuka na Majanga hayo.

 

Related Posts