Jenerali Mkunda awavisha nishani Maafisa wa JWTZ

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Jacob Mkunda amewavisha nishani za hadhi mbalimbali baadhi ya watumishi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu.

Hafla ya uvalishaji wa nishani hizo imefanyika mkoani Morogoro ambapo miongoni mwa nishani zilizovishwa ni pamoja na Nishani ya Utumishi Mrefu Jeshini, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, Nishani ya Miaka 60 ya Muungano na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.

Nishani hizo zimevalishwa kwa baadhi ya majenerali wenye vyeo vya ngazi mbalimbali, maafisa na askari wa JWTZ.

Related Posts