Pascal William bosi mpya Mainstream Media Ltd

 

KAMPUNI ya Mainstream Media imeteua Pascal William kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Mauzo na Usambazaji, kuanzia tarehe 10 Septemba 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uteuzi huo umetajwa kuwa umetokana na rekodi nzuri ya William kwa kuwa kiongozi mwenye mikakati katika mauzo na usambazaji.

Akitangaza uteuzi wake, Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Deogratius Mosha amesema William ataleta utaalamu na uzoefu mkubwa alionao katika sekta za mawasiliano na benki nchini.

Amesema historia yake inamfanya kuwa rasilimali muhimu kwa timu yao na yuko tayari kupeleka mipango ya mauzo mbele.

“Kazi inayofanywa na William imekuwa na michango mkubwa kwa timu zilizofanikiwa kuongozwa naye kwani amekuwa akileta matokeo ya kipekee na ya kuvutia.

“Ufahamu wake mkubwa wa kuboresha michakato ya mauzo na kuongoza mipango ya ukuaji wa kimkakati ni ya kuvutia sana, haswa wakati wa kipindi chake katika sekta ya benki, ambapo alichangia sana katika kuboresha mauzo na usambazaji,” amesema.

Amesema wanafurahi kutumia uongozi na uzoefu wa William kufikia malengo yao ya ukuaji kama kampuni.

About The Author

Related Posts