Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima, amewataka wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Mazingira kuchangamkia fursa ya Maonesho Makubwa ya Kilimo Biashara yanayotarajiwa kufanyika Wilayani Gairo kuanzia Oktoba 06, 2024 hadi Oktoba 12, 2024.
Rai hiyo ameitoa Leo wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia Maonesho hayo ambayo yatawaleta pamoja wadau wote wanaohusika katika Mnyororo wa Thamani wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Mazingira wakiwemo Wakulima na Wafugaji , Wauzaji na Wazalishaji wa Pembejeo za Kilimo na Mifugo, Taasisi za Fedha, Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo na Mifugo, Wasindikaji na Wafanyabiashara, Mashirika ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali yanayojihusisha na Shughuli za Kilimo, Mifugo na Mazingira, Taasisi za Umma na Binafsi zinazotoa Huduma ambatano kwa wakulima na wafugaji ikiwemo Taasisi za Bima, Hifadhi ya Jamii, Nishati Safi ya Kupikia, nk
Aidha, Mhe. Malima amewataka wakulima na wafugaji kuchangamkia fursa hiyo kwenda kujifunza mbinu na Teknolojia Bora na za kisasa za Ufugaji na Kilimo Bora ili iwasaidie katika kupambana na umasikini, kwani Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania amewekeza vya kutosha katika Kilimo na Mifugo ili kuzifanya Sekta hizo kukua na kuwakomboa wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame alisema zaidi ya asilimia 95 ya Wananchi wa Gairo wanajishughulisha katika Sekta ya Kilimo na Mifugo hivyo Sekta hizi ndiyo muhimili wa kukuza Pato la Mwananchi mmoja mmoja, kukuza uchumi wa Wilaya na Kuongeza Ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha, Maonesho haya yatatanguliwa na Mikutano muhimu miwili ya Wakulima na Wafugaji ambayo ni 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐌𝐈𝐅𝐔𝐆𝐎 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐅𝐎𝐑𝐔𝐌 𝐮𝐭𝐚𝐤𝐚𝐨𝐟𝐚𝐧𝐲𝐢𝐤𝐚 𝐒𝐞𝐩𝐭𝐞𝐦𝐛𝐚 19, 2024 𝐧𝐚 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐅𝐎𝐑𝐔𝐌 – 𝐇𝐎𝐑𝐓𝐈𝐂𝐔𝐋𝐓𝐔𝐑𝐄 (𝐌𝐁𝐎𝐆𝐀𝐌𝐁𝐎𝐆𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐓𝐔𝐍𝐃𝐀) 𝐮𝐭𝐚𝐤𝐚𝐨𝐟𝐚𝐧𝐲𝐢𝐤𝐚 𝐎𝐤𝐭𝐨𝐛𝐚 24 𝐧𝐚 25, 2024.
Mikutano hii itatoa fursa kwa wakulima na wafugaji kujadiliana, kujengewa uwezo na kubadilishana uzoefu wa mbinu Bora na Teknolojia za Kisasa katika Ufugaji na Sekta ya Kilimo Cha Mbogamboga na Matunda ikiwemo zao la Parachichi na Viazi Mviringo. *Hatua hii ni utekelezaji wa maono Makubwa ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta Mageuzi katika Sekta ya Kilimo na Mifugo kupitia Mkakati wa Ajenda 10/30 ambao unalenga kuongeza Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Kilimo kufika Asilimia 10% mwaka 2030 kutoka Asilimia 4.2% Mwaka 2023.*
Maonesho ya “SAMIA KILIMO BIASHARA EXPO 2024” yamebeba ajenda Kuu 5 ambazo ni Ushiriki wa Wananchi Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara, Nishati Safi ya Kupikia na Fursa ya Biashara ya Kaboni, Afya na Lishe, Ushirika na Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
Maonesho haya yamebeba Kauli Mbinu isemayo;- *“TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA MAENDELEO YA KILIMO NA MIFUGO”*