Trump anusurika tena kupigwa risasi, adai hakuna cha kumpunguza kasi

Vyombo vya habari vya New York Times, Reuters na Fox News vimemtaja, Ryan Routh (58) kuhusika na tukio la kujaribu kumpiga risasi Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais kupitia chama Cha Republican, Donald Trump jana.

Hii inakuwa mara ya pili kwa Trump kunusurika kifo kwenye mashambulio ya risasi katika kipindi hiki cha kampeni za nchi hiyo. Awali Julai 13, 2024 alikumbana na tukio kama hilo wakati akihutubia Butler.

Routh ambaye bado Shirika la Ujasusi la nchi hiyo (FBI) halijamthibitisha, anadaiwa kufyatua risasi hiyo jana Jumapili Septemba 15, 2024, akimlenga Trump aliyekuwa akicheza Golf kwenye uwanja wake wa Golf wa kimataifa uliopo West Palm Beach.

Reauters imeripoti kuwa Routh alishtukiwa mapema na walinzi wa Trump kabla hajaleta madhara na  alikimbia kabla ya kukamatwa, huku FBI wakisema wanaendelea na uchunguzi.
Baada ya tukio hilo, Trump kupitia ofisi yake binafsi ametoa taarifa kwa umma kuwa yupo salama.

“Kuna risasi zilipigwa karibu na eneo nilipokuwa, lakini kabla ya uvumi kusambaa nataka kuwafahamisha kuwa nipo salama na mzima, hakuna kitachonipunguza kasi,”amesema Trump ambaye yupo kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais na Kamala Harris wa Democratic

Related Posts