Wakazi wa Kariakoo Wazindua Mradi Kigamboni

Na Mwandishi Wetu

UMOJA wa wakazi wa Kariakoo wamezindua mradi wao wa maendeleo katika Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Wakazi hao kupitia taasisi yao iitwayo Kariakoo Development Family Foundation, wamezindua mradi huo uliopo mtaa wa Vumilia Ukooni, kata ya Kisarawe I|, wenye lengo la kufuga kuku pamoja na bwala la samaki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Stephano Waryioba amewataka kufungua fursa kwa wenyeji wa maeneo hayo ili waweze kunufaika na miradi hiyo pamoja na kubadilishana uzoefu ili kujikwamua kiuchumi.

” Kwanza niwakaribishe sana Kigamboni, ofisi yangu ipo wazi saa 24 kuwahudumia mkiwa na jambo lolote.

“Niwaombe mkae na wenyeji vizuri mshirikiane na kubadilishana uzoefu, naamini na wao wana kitu mnaweza kusaidiana,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo ya Kariakoo Development Family Foundation, Mohamed Bhinda, amesema wanatarajia kuanza mrdai huo mara moja baada ya baadhi ya taratibu kukamilika.

” Kiukweli hatutakuwa na muda mrefu wa kuanza kwa miradi hii ya kufuga kuku pamoja na bwala la samaki, hivyo tunaamini mambo yataenda sawa.

“Tumekuja kuwekeza Kigamboni kwa sababu ni karibu na Kariakoo ni rahisi kufika, lakini pia hali ya hewa nzuri,” alisema.

Bhinda aliwashukuru wakazi wa mtaa huo kwa ukarimu wao wa kuwakaribisha na ushirikiano waliouonesha na amewaomba washirikiane nao katika maendeleo ya kiuchumi.

Bhinda pia aliishukuru Serikali ya mtaa huo wa Vumilia Ukooni kwa kuwapokea vizuri na wameahidi kushirikiana nao katika kuleta maendeleo.

Tayari taasisi hiyo imekubali kuwa walezi wa kikundi cha hamasa cha mtaa huo, ambao walitoa burudani katika uzinduzi huo.

Related Posts