Na Mwandishi Wetu
Mhashamu Askofu Mkuu wa Anglikan Catholic church Duniani Mark Hervland ameimbia serikali kuwa Kanisa liko tayari kushirikiana nayo katika kutatua changamoto mbalimbali za huduma za jamii zinazo wakabili Wananchi hasa ujenzi wa Miundombinu ya maji sehemu za Vijijini ili wapete maji safi na tiririka
Mhasham Askofu Harvland amayasema hayo kijijini Mlali wilayani Kongwa kwenye Misa takatifu ya kumsimika Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa hilo Jimbo la Tanzania Dr Elibariki Philip KUTTA .
Aidha Askofu Harvard amefafanua kuwa wakati wa ziara yao wiki iliyopita katika Wilaya za Mpwapwa na Kongwa wameshuhudia shida ya Maji katika Wilaya hizo hasa sehemu za Vijijini na kiahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kumtua ndoo Mama Kichwani
Ameeleza kuwa shida ya Maji inasababisha Wananchi wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi kwa kutumia muda kutafuta maji pia na kushindwa kuhudhuria ibada na mafundisho ya dini kwa sababu ya kutafuta maji hasa nyakati za kiangazi
Ameongeza kuwa anatamani kuona maji yanamfuata mwananchi na sio mwananchi anafuata maji na kila nyumba kwenye Wilaya hizo zina kuwa na bomba la maji na mradi unanzia kwenye kijiji cha Mlali wilayani Kongwa
Katika hatua nyingine Askofu Harvland Ameahidi kumsaidia Askofu Dr Elibariki KUTTA kuanzisha miradi ya huduma za kijamii Elimu Afya, Kilimo na ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa michezo katika Kijiji cha Mlali wilayani Kongwa pamoja na ujenzi wa Zahanati miradi hiyo inakamika kwa wakati,
Kwenye hotuba yake ya shukran Askofu Kutta amemshukuru Askofu Mkuu Mark Hervland kwa kuwajali Wananchi wa Tanzania hasa waishio vijijini.