Jesca afunika DBL | Mwanaspoti

Katika michezo, suala la kucheza rafu ‘madhambi’ ni kawaida na ndiyo maana kumewekwa sheria na adhabu zitolewazo kutokana na mchezaji kufanya vitendo visivyokubalika.

Kwenye soka, mifano ipo mingi kwa nyota wake ambao kuna waliocheza kwa miaka mingi na hadi wanastaafu hawajui kadi.

Licha ya kutumikia nafasi ngumu uwanjani ambayo wanaoitumikia hukumbana na kucheza rafu lakini kwa beki wa zamani wa Maji Maji ya Songea, Samli Ayubu hajawahi kukumbana na adhabu na hakuwa anapenda kucheza rafu.

Ni sawa na Chipukizi wa mpira wa kikapu, Jesca Lenga anayeichezea DB Troncatti inayoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Dar es Salaam (DBL).

Jesca hadi sasa amecheza michezo 27, bila ya kufanya madhambi wala kuonywa na mwamuzi licha ya kucheza nafasi ya kati ‘pointi guard’.

Mwanaspoti lilikuwepo viwanja vya Donbosco Upanga na lilimuuliza mmoja wa waamuzi wa ligi hiyo, Oscar Chrispin Komba kuhusu sifa hiyo kwa Jesca na alisema kinachombeba ni nidhamu aliyokuwa nayo ya ukabaji.

Alisema ni mchezaji mwenye uwezo na mzuri kwenye kushambulia na kutoa pasi za mwisho ‘assist’ na ni ngumu kumkaba.

Related Posts