Srelio yaiweka Pabaya Crows | Mwanaspoti

SRELIO imeichapa Crows pointi 74-72 katika Ligi ya Mpira wa kikapu Dar es Salaam (BDL), kwenye uwanja wa Donbosco, Upanga na kuiweka katika nafasi mbaya ya kushuka daraja msimu huu.

Hata hivyo licha ya kupoteza mchezo huo, Crows ilionyesha kiwango kizuri katika robo zote nne na iliongoza robo ya kwanza kwa pointi 19-13, huku robo ya pili na ya tatu Srelio iliongoza kwa pointi 20-15, 25-20, 16-18.

Hata hivyo, Charly Kesseng wa Srelio ndiye aliyekuwa kizingiti kikubwa kwa Crows kutokana udakaji wake wa mipira ya ‘rebounder’ iliyofika eneo lake, huku pia akiongoza kwa ufungaji na alifunga pointi 23, ikiwamo ya mitupo mitatu ‘three points’ mara tatu, akifuatiwa na Boniface Chami aliyefunga pointi 15.

Kwa upande wa Crows, Christopher Kinoti ndiye aliyefunga  pointi 17, huku Charles Alson akifunga pointi 14.

Related Posts