Bunge laanzisha mchakato kumwondoa Rais Macron

 

OFISI ya Bunge la taifa Jumanne Septema 17, 2024 imetoka taarifa juu mchakato wa kutimuliwa kwa Rais Emmanuel Macron uliowasilishwa na baadhi ya waunge wa chama cha New Popular Front.

Wakati Ufaransa inasubiri serikali yake mpya kwa miezi miwili, chama cha NFP kimesema kwamba mkuu wa nchi anafanya “mapinduzi dhidi ya demokrasia”. Hata hivyo, utaratibu huu unaoneakana kutokuwa na nafasi ya kufanikiwa.

Ofisi ya Bunge ndiyo imekamilisha mkutano wake na sasa na imethibitisha: azimio lililopendekezwa linalolenga kumtimua mamlakani Macron kwamba litaendelea na mkondo wake katika Baraza la Bunge.

Huku NFP ikiwa na wingi wa kura katika ofisi ya Bunge, azimio hilo limepitishwa kwa kura 12 dhidi ya 10.

Huu ni wakati ambao haujawahi kushuhudiwa chini ya Jamhuri ya 5 kwa sababu hapo awali hakuna utaratibu wa kumtimua kiongozi wa nchi uliwahi kufika mbali kama sasa.

Miaka 10 iliyopita, pendekezo lililowasilishwa na mrengo wa kulia dhidi ya François Hollande lilikataliwa katika hatua ya ofisi hiyo.

About The Author

Related Posts