Geita DC, yatangaza maeneo ya kiutawala katika vijiji na vitongoji

Halmashauri ya wilaya ya Geita imetangaza rasmi Maeneo ya Kiutawala Majina ya Mipaka ya Vijiji na Vitongoji katika Maeneo majimbo likiwemo Jimbo la Busanda na Jimbo la Geita katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Akitangaza Maeneo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Rajabu Kalia amesema lengo la kufanya vile ni kumfahamisha mwananchi kujua eneo lake la kiutawala sambamba na kutambua viongozi halisi wa Maeneo yake.

“Sheria za Serikali za Mitaa chini ya Mamlaka ya wilaya sura namba 287 kwa Mujibu sura namba 188 zinaelekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa lengo ni kuzifanya serikali za Mitaa ziongozwe kwenye Demokrasia, ” Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Geita , Kalia.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 101 cha Sheria za Serikali za Mitaa mamlka ya wilaya sura namba 287 na Kifungu cha 87 a cha sheria za Serikali za Mitaa mamlaka za Miji ambayo ni sura namba 288 Waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa ana mamlka ya kutunga kanuni za Uchaguzi za Serikali za Mitaaanapohitajika kuongoza uchaguzi huo, ” Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Geita, Kalia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita , Charles Kazungu amewataka viongozi mbalimbali wakiwemo Maafisa katika Zoezi kuacha Mzaa kwani Jambo hilo ni la kitaifa na haliitaji kuwekewa mzaa wa aina yoyote.

“Rai yangu tuu kwenu tumeanza tukio hili ni tukio muhimu sana la kitaifa linahitaji weredi linahitaji kiwacha Mizaa yote kama mulikuwa na mizaa kwa maafisa wenu wa halmashauri sasa hili ni jambo la Kitaifa.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya wilaya ya Geita ina kata 37 , Vijiji 145 na Vitongoji 593 ambavyo tayari vimekwisha kugawika katika maeneo mbalimbali ya kiutawala.

Related Posts