MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA MAHAKAMA UMECHANGIA KUPUNGUZA MLUNDIKO WA KESI

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

MATUMIZI ya TEHAMA katika Mahakama mbalimbali hapa nchini,umechangia kupunguza mlundikano wa kesi katika mahakama kutoka asilimia 10 hadi tatu mpaka kufikia mwaka jana.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 18 Septemba, 2024 na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akifungua Semina juu ya Maboresho na Uongozi wa Kimkakati katika Mnyororo wa Utoaji Haki kwa Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) iliyofanyika katika Hoteli ya ‘African Dreams’ jijini Dodoma.

Profesa Ole Gabriel amesema tathmini hiyo hutolewa kila baada ya miaka minne na taasisi hiyo,hivyo suala la TEHAMA linazidi kupunguza msongamabo mahakamani.

“Tunashukuru matumizi ya TEHAMA katika mahakama kunasaidia kwa kiasi kikubwa kuounguza mlundikano wa mashauri tunaendelea kutumia TEHAMA ili kurahisisha uendeshaji wa kesi,”alisema Profesa Ole Gabriel.

Amesema wanasubiri tathmini nyingine ambayo itatolewa baada ya miaka minne na kuongeza kuwa,wanaishkuru sana serikali Kwa kuwekeza katika mahakama.

Mbali na hilo amesema,wamepokea ombi la TLS la kuwataka mahakama kutoa elimu kwa mawakali kuanzia juu hadi ngazi ya chini ili kusaidia nao wajue mifumo inayotumika.

Amesema wao kama Mahakama wamelipokea na watalifanyia kazi ili kihakikisha uhusiano wao u akwenda vizuri katika masuala ya kisheria.

Hata hivyo Mahakama Tanzania wamealikwa kwenda Marekani ili kuelezea namna wanavyotumia mikopo nafuu katika uwekezaji wa mahakama uliopelekea kuounguza mlundikano wa.kesi mahalamani.

Amesema mualiko huo no hatua kubwa kwao na kuongeza kuwa utazidi kupanua wigo wa Ufanyaji kazi ya mahakama.

Mbali na hayo amesema watasaidia MOU Kwa ajili ya kushirikiana na Baraza la TLS ili kihakikisha kila mmoja anapata haki yake.

Naye Rais wa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi amesema wameiomba Mahakama kutoa elimu zaidi kwa mawakili ili waweze kukaa boti moja katika masula ya kisheria na utensaji kazi.

TLS wamewasilisha ombi hilo ili kuona kama litafanikiwa ili iwe rahisi kwao kufanya kazi zao kwa urahisi kutokana na kuwa kila siku wanakutana na kesi.

Wakili Mwabukusi amesema mahakama ni sehemu ya.kupata haki,hivyo anaye ilalamikia mahakama anahitaji kuchunguzwa kutokana na kuwa mahakama haimuonei mtu.

Hata hivyo Mwambukusi amesema anaamini ushirikiano huo utakwenda kuleta matokeo chanya Kwa jamii inayotuzunguka kwenye masuala ya kisheria hapa nchini.




Related Posts