Nyasebwa: Ushindani mwanza ni mkubwa

Kocha wa mchezo wa Kikapu Mkoa wa Mwanza, Benson Nyasebwa amesema ushindani wa ligi hiyo mkoani humo ni mkubwa.

Nyasebwa aliliambia Mwanaspoti, ushindani huo unatokana na viwango vikubwa vinavyoonyeshwa na timu zote zinazoshiriki ligi hiyo.

Wakati huo huo, Planet iliifunga Crossover kwa pointi 59-49 katika mchezo wa ligi ya mkoa wa Mwanza katika Uwanja wa Mirongo.

Mchezaji Romanus wa Planet aliongoza kwa kufunga pointi 14, huku kwa upande wa udakaji wa mipira ‘rebounder’ alidaka mara tano na kuasisti mara mbili.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uwanjani hapo, Sengerema iliifunga CUHAS kwa pointi 54-42.

Related Posts