REA yamtambulisha mkandarasi wa kutekeleza mradi wa zaidi ya Bilioni 14 mkoani Kagera

Wakala wa nishati Vijijini (REA) kupitia Meneja wake wa Kanda ya Ziwa Mhandisi Erenest Makale wamemtambulisha mkandarasi kwa ajili ya kuanza zoezi la kusambaza umeme kwenye vitongoji 135 vya Mkoa wa Kagera.

Zoezi hilo limefanyika katika kata ya Katerero iliyopo Wilaya ya Bukoba huku likishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa ambaye amemtaka Mkandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya CCIC kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha unakamilika kwa muda uliopangwa.

Aidha amewaagiza REA kupeleka kambi ya watumishi wa kutosha kusimamia mradi huo ili kabla ya uchaguzi mkuu ujao vitongoji vyote viwe vimefikiwa na umeme.

Kwa upande wake Meneja wa REA kanda ya ziwa Mhandisi Erenest Makale amesema kuwa mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 14 za Kitanzania,na kazi kubwa inayofanyika ni kujenga transfoma na kuanza kusambaza umeme kwa wananchi ambao wamelengwa huku akiongeza kuwa kwa Mkoa wa Kagera wamelenga kufikia vitongoji 135 na kila jimbo litakuwa na vitongoji 15.

Related Posts