ZAIDI YA WANANCHI 4300 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI NDELENYUMA RUVUMA








BELINDA JOSEPH SONGEA
WANANCHI zaidi ya elfu 4 wanatarajia kunufaika na huduma ya maji safi na salama, kufuatia Mradi wa Maji wa Bilioni 1.6 ambao umefikia asilimia 86.7 unaotekelezwa na Wakala wa maji safi na mazingira Vijijini RUWASA, mradi unaotarajiwa kukamilika mwezi oktoba mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mathias P Charles wakati akitoa taarifa za mradi huo mbele ya wananchi wa Kijiji cha Ndelenyuma kata ya Mkongotema Halimashauri ya Madaba katika mwendelezo wa ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso Mkoani Ruvuma.
Nae Waziri wa Maji Jumaa Aweso mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo, amesema miradi ya maji inayotekelezwa nchini inalenga kuwatua kinamama ndoo kichwani kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji hii yote inatokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassani kuhakikisha suluhu ya changamoto za maji inapatikana.
Amewataka wananchi wa eneo hilo kuulinda na kuutunza mradi wa maji kutokana na kuondoa adha ya kuamka alfajiri kufuata maji maeneo ya mbali huku matarajio yake kupitia mradi huo kutaongeza uzalishaji wa viti mbalimbali pamoja nakurahisisha huduma za kijamii.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wameeleza kuwa mradi huo pindi utakapokamilika utasaidia kuepuka changamoto ya ukosefu wa maji katika msimu wa kiangazi hivyo matarajio ni makubwa kwao kupata maji ya uhakika.
Kadharika kinamama wamesema kutokuwepo kwa maji katika eneo inawalazimu kwenda katika vituo vya afya na ndoo za maji kipindi cha kujifungua jambo ambalo wanaamini Mara tu mradi huo utakapokamilika kutakuwa na urahisi wa huduma hiyo ambayo wanategemea itaunganishwa moja kwa moja katika vituo vya afya.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Mhe. Joseph Kizito Mhagama ameeleza kuwa hadi hivi Sasa hakuna kijiji Madaba ambacho hakina mradi wa maji, ambapo amempingeza Rais pamoja na Wizara ya Maji kuendelea kupeleka miradi ya maji jimboni kwake.

Related Posts