AKILI ZA KIJIWENI: Afrika Mashariki tuitendee haki Chan

RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Patrice Motsepe hivi karibuni alitangaza habari njema ambayo nchi za Tanzania,  Kenya na  Uganda hapana zingeifurahia.

Motsepe alitangaza fainali za mataifa ya Afrika zinazohusisha wachezaji wanaocheza katika Ligi za Ndani (Chan) zitafanyika mwakani katika nchi hizo kuanzia Februari Mosi hadi 28 mwakani.

Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuandaa fainali hizo za Chan baada ya kufanyika katika nchi ya Sudan mwaka 2011 na nyingine kufanyika Rwanda 2016.

Hata hivyo, nchi za Uganda, Tanzania na Kenya zinapaswa kujipanga vilivyo katika maandalizi ya fainali hizo zijazo za Chan mwakani ili ziweze kufanyika katika kiwango na ubora wa hali ya juu ambao kwa kiasi kikubwa utachangia kuishawishi Caf kubakisha haki ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2026 zitakazofanyika katika hizo nchi tatu.

Tuyape thamani kubwa mashindano ya Chan mwakani kwa vile yana nafasi kubwa ya kuamua kama tutaweza kuandaa Afcon mwaka 2027 au haitowezekana kulingana na tathmini ambayo itafanywa na timu ya wataalam kutoka Caf.

Tujitahidi kujitokeza kwa wingi viwanjani katika mechi mbalimbali za Chan  ambazo zitachezwa katika siku za hivi karibuni ili kuonyesha kuwa Afrika Mashariki kuna hamasa na msisimko wa soka kwa mashabiki.

Tuboreshe miundombinu yetu kama vile viwanja vya mechi, mazoezi na barabara ili iweze kutimiza mahitaji yanayotakiwa na Caf kwa nchi mwenyeji wa mashindano yake makubwa na sio tungojee tufanye kwake

Kuanzia sasa hadi Februari Mosi na fainali za Chan zitaanza kufanyika ni muda wa takribani miezi mitano umebakia kabla ya nchi zetu tatu, Kenya, Tanzania na Uganda kuandaa Chan kwa mujibu wa kalenda ya Caf.

Muda huu uliobakia tunaweza kuuona mwingi lakini kiuhalisia ni mfupi sana kuweza kukamilisha vitu vyote vya msingi ambavyo vinahitajika ili haki ya uenyeji wa Chan ibakie katika ukanda wetu msimu huu.

Related Posts