DC MPOGOLO ATAKA VIONGOZI KUWA NA MAHUSIANO MEMA

 

 Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi wa chama na serikali kuwa na mahusiano mazuri katika kazi zao.

Akiongea na viongozi wa chama na serikali katika ziara yake kwenye kata ya liwiti, tabata na kimanga Mpogolo ameeleza mahusiano ya viongozi hao yanasaidia kuelewa kazi zinazofanywa katika miradi ya maendeleo hivyo wasione ugeni kushirikiana.

Ameongeza kuwa hata katiba ya nchi inatambua mahusiano na mfumo wa chama chenye dhamana  na serikali iliyopo madarani kupitia ilani inayotekelezeka. 

Akielezea kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu amewataka wananchi kushiriki, kujiandikisha na kupiga kura na kudumisha umoja, upendo na mshikamano.

 Amesema viongozi wahamasishe wananchi kujiandikisha katika daftari litalikuwa katika maeneo ya mitaa wanayoishi zoezi ambalo litaanza tarehe 11 hadi 20 mwezi ujao na uchaguzi ni novemba 27 mwaka huu. 

Akijibu kero zilizowasilishwa katika mkutano uwo Mpogolo amesema kero zinazohusu elimu hasa uzio katika shule ya sekondari liwiti iliyopakana na shule mbili za msingi halmashauri itahakikisha inatatuliwa kwa wakati. 

Kero nyingine aliyoitolea ufafanuzi ni kuhusu mto msimbazi ambao ni kilio kwa wananchi na serikali tayari imeona na kuanza kutafuta njia ya kuondoa kero hiyo kwa kuwa mto uwo umekuwa na tabia ya kuhama hama. 

Kuhusu kero ya barabara katika kata ya tabata, liwiti na kimanga ameleeza barabara hizo zipo zilizoingia katika mradi wa Dmpd na nyingine zitashughulikiwa na tarura.

Aidha Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi, wazazi na walezi kusimamia maadili ya watoto kwa ujumla hasa waliomaliza darasa la saba wasipate mimba na magonjwa ya zinaa.

Related Posts