DK.JAFO APIGA MAARUFUKU KUCHANGANYA MAZAO

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama  wakitembelea na kukagua Ghala la Mpako linalotumia Mfumo wa Stakabadhi liilopo Wilaya ya Liwale ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Maalum katika Mkoa wa  Lindi kwa lengo kukagua utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

…..

WAZIRI  wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo  ametoa rai kwa Watanzania kuacha kuchanganya mazao ili kutokuharibu au kupunguza thamani ya mazao hayo katika soko la kimataifa na kuharibu taswira ya Tanzania.

Dkt.Jafo ameyasem ahayo mara baada ya kutembelea  Ghala la Mpako linalotumia Mfumo wa Stakabadhi ghalani wakati wa ziara yake  maalum Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kuongea na Wananchi wa Maeneo hayo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Aidha ameliagizza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuendelea kusimamia na kufuatilia ubora wa Mazao hayo yanayohifadhiwa na kuuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani na Wakala wa Vipimo (WMA) kuhakikisha mizani zote nchini zinapima mazao kwa usahihi

“Nimeridhika na ujenzi wa ghala hili niwaombe sana watanzania muache kuchanganya mazao ndugu zangu hivyo naiagiza Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) ndani ya siku 20 kukaa kikao na Bodi ya Korosho ili kufanya tathimini ya siku ngapi zinafaa kutoa korosho gharani huku wakifanya utafiti wa kina kuhusu suala la unyaufu katika zao la Korosho ili kuhakikisha wananchi wanafaidika na mazao yao ya kilimo.”amesema Dkt.Jafo

Aidha, katika ziara yake Wilayani humo amebainisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ujenzi shule za sekondari na zahanati imetumika vizuri na miradi hiyo imejengwa katika kiwango kinachohitajika na amewataka Watoto wa shule hizo kusoma kwa bidii ili wawe viongozi wa siku zijazo.

Waziri Jafo alikagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Kichonda, pamoja na kuweka  jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Ngorongopa, jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Bweni la Watoto Maalum katika shule ya Msingi Kambarage na alizindua jengo la vyumba 3 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo katika shule ya Msingi Luiza Mlelwa.

Akiongea na Wananchi wa Liwale Dkt Jafo amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendele kutatua changamoto mbalimbali walizonazo ikiwemo kuweka mindominu wezesheshi ya barabara , maji na umeme ili luhakikisha uchumi wa nchi hii inaongea na kukuza uchuma

Naye Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe Goodluck Mlinga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kuwa Wilaya yake itaendelea kusimamia Miradi hiyo kikamilifu na kuwataka Wananchi wa Wilaya hiyo kutumia fursa za miradi hiyo ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla. Wananchi na watoto wa lowale wanapata huduma stahiki wamepokea vifaa vya kisaaa

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Bw. Asangye Bangu alibaimisha kuwa atatekeleza maelekezo yaliyotolewa na kuwataka Wananchi kuendelea kutumia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani unaowawezesha wakulima kuuza mazao hayo kwa bei nzuri na kuwataka Wananchi hao kuweka ghalani mazao yenye ubora unaotakiwa.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kukagua  ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Kichonda Wilaya ya Liwale  wakati wa ziara Maalum wilayani  humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi  mara baada ya kukagua  ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Kichonda Wilaya ya Liwale  wakati wa ziara Maalum wilayani  humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na Viongozi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Liwale  akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Ngorongopa, Wilaya ya Liwale wakati wa ziara Maalum wilayani  humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka  jiwe la msingi ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Ngorongopa, Wilaya ya Liwale wakati wa ziara Maalum wilayani  humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama  wakitembelea na kukagua Ghala la Mpako linalotumia Mfumo wa Stakabadhi liilopo Wilaya ya Liwale ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Maalum katika Mkoa wa  Lindi kwa lengo kukagua utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Liwale katika Mkutano wa Hadhara wenye lengo la kusikiliza changamoto zao  ikiwa ni mwendelezo wa ziara Maalum Mkoani Lindi kwa lengo la  kukagua utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo ,akizungumza  na walimu na wanafunzi mara baada ya kuzindua  jengo la vyumba 3 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo katika shule ya Msingi Luiza Mlelwa iliyopo Wilaya ya Liwale wakati wa ziara yake Maalum Mkoani Lindi yenye  lengo kukagua utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone

 

Related Posts