KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA KIFO CHA MZEE S. T. NATHAN

 

Ni Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika 17 sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani.

Nimajonzi sana kwetu na pengo lako halijazibika hadi hivi leo.

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee unakunbukwa na Mke wako Mary O Nathan  pamoja na watoto wako wote, wakwe zako, wajukuu wako na vitukuu.

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Same na Ugweno mkoani Kilimanjaro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko yako. 

Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo daima.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

 

Related Posts