Picha :Mndeme afanya uhamasisahi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia Rukwa

NAIBU Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Christina Mndeme ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan juu ya kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Mndeme katika kuunga juhudu hizo ameanza ziara iliyo na lengo la kutoa elimu hiyo mikoa yote Tanzania ambapo kwa sasa mikoa itakayonufaika na elimu ya Nishati Safi ya Kupikia ni pamoja na Rukwa, Songwe, Mbeya na Njombe.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere wakati wa ziara yake mkoani humo alipokuwenda kutoaji elimu na uhamasisahi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambapo mikoa mitano itanufaika na elimu hiyo ikiwemo Songwe, Mbeya na Njombe na tayari ametoa Rukwa na Katavi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere akizungumza na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (kulia) alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya utoaji elimu na uhamasisahi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambapo mikoa mitano itanufaika na elimu hiyo ikiwemo Songwe, Mbeya na Njombe na tayari ametoa Rukwa na Katavi.


Wadau mbalimbali wa Nishati Safi ya Kupikia Sumbawanga mkoani Rukwa wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (hayupo kwenye picha) alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya utoaji elimu na uhamasisahi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambapo mikoa mitano itanufaika na elimu hiyo ikiwemo Songwe, Mbeya na Njombe na tayari ametoa Rukwa na Katavi.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme akigawa chakula kwa mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga mkoani Rukwa mara baada ya kwenda chuoni hapo kuangalia mwitikio wa taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 walivyoanza kuitikia wito wa Serikali wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambapo chuo hicho kinatumia Mkaa Mbadala.

Related Posts