Profile ilizinduka katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mwanza baada ya kuifunga Oratorio kwa pointi 71-40 kwenye Uwanja wa Mirongo.
Profile katika mchezo wao, Jumapili iliyopita ilifungwa na Planet kwa pointi 49-43, huku Oratory ikifungwa na CUHAS kwa pointi 58-46 na Zakayo Omugo wa Profile aliongoza kwa kufunga pointi 18.
Eagle iliifunga Young Profile kwa pointi 49-43 katika mchezo ulikuwa mzuri na wa kupendeza kwenye uwanja huo.
Jumapili iliyopita Eagle iliifunga Sengerema Hoopers kwa pointi 52-49.
Eagle ilianza mashindano hayo kwa kufungwa mara mbili na Planet kwa pointi 62-59, 81-71.