Rabia ateta na Naibu Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Common Wealth Foundation jijini London

Tarehe 18 Septemba, 2024 Jiji London Uingereza, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa amefanya mazungumzo na Bw. Shem Ochola, Naibu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Common wealth Foundation ambaye aliambatana na Bi. Sheila Ruiz, Meneja wa Uhamasishaji na Ubunifu kutoka katika taasisi hiyo.

Katika Mazungumzo hayo Bw. Ochola na Bi. Sheila Ruiz wamemuleza Ndugu Rabia shughuli mbalimbali zinazofanya na Taasisi ya Commonwealth Foundation ikiwemo ni pamoja na kuhamasisha masuala ya utunzaji wa mazingira, Uboreshaji wa huduma za afya, kukuza demokrasia, uwajibikaji, usawa wa kijinsia, na haki za binadamu.


Kwa Tanzania taasisi hiyo kupitia asasi za kiraia inafadhili miradi mbalimbali inayowasaidia wakulima wadogo wadogo kuboresha uzalishaji kwa kutumia mbinu za kilimo kinacholinda mazingira na matumizi ya teknolojia bora zinazopunguza uharibifu wa ardhi na misitu.

Kwa upande wa utunzaji wa mazigira taasisis hiyo inafadhili baadhi ya asasi za kirai zilizojikita katika utunzaji wa vyanzo vya maji, upandaji wa miti, na juhudi za kukabiliana na uharibifu wa misitu ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, kusaidia kuhifadhi bayoanuwai, na kuimarisha juhudi za upunguzaji wa hewa ukaa
Kwa upande wake, Ndugu. Rabia amelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na CCM chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amefafanua kuhusu falsafa ya Mhe. Rais ya R nne, yaani Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mabadiliko), na Rebuilding (Ujenzi upya) jinsi zilizosaidi kuimarisha umoja wa kitaifa na kuwaunganisha Watanzania .

Aidha ameelezea hatua zinazochukuliwa na serikali inayongozwa na CCM katika masuala ya utunzaji wa mazingira. Amewajulisha kuwa suala la uhifadhi wa mazingira ni suala linalopewa kipaumbele cha pekee na Mhe. Rais Mwenyewe na katika kuhakikisha Tanzania inatokomeza ukatajiwa wa miti kwa ajili ya nishati ya kupikia, Mhe. Rais amekuwa ni kinara wa kampeni ya Clean Cooking barani Afrika yenye lengo kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa ili kuhifadhi mazingira.

Ndugu. Rabia pia amesema kwamba serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuboresha huduma za afya, elimu, pamoja na kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi.

Pia alisisitiza kuhusu juhudi za serikali katika kuimarisha masuala ya usawa wa kijinsia, kuhakikisha fursa sawa kwa watu wote bila kujali jinsia au umri.

Ndugu Rabia ameihakikishia taasisi ya Commonwealth Foundation kuwa serikali inyaongozwa na CCM itandelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa katika masuala ya maendelea na mambo mengine muhimu yenye manufaa kwa pande zote mbili.

Related Posts