Tano zaombeana mabaya LIGI DAR

WAKATI timu zikiwa zimebakiza michezo miwili zikamilishe michezo 30  ya mzunguko wa pili wa Ligi ya Mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), imeonekana ushindani utakuwa   kwa timu tano zinazopambana kujinasua zisishuke daraja.

Timu hizo ni KIUT yenye pointi 34, Mgulani JKT (33), Jogoo (33), Crows (32), Chui (29).

Kati ya timu hizo, imeonyesha Chui ndiyo yenye nafasi kubwa ya kupenya kujinasua kushuka daraja kutokana na viporo saba ilivyonavyo.

Nafasi ya timu  hiyo kupenya, itaanzia kupewa  pointi saba endapo watapoteza michezo saba itakayofanya wapate pointi 35, huku  timu hiyo ikiombea zingine zipoteze michezo yake.  

Sheria ya matokeo ya mchezo wa kikapu inaeleza, endao timu itashinda itapewa  pointi mbili ikifungwa inapata pointi moja.

Timu zilizotinga kucheza  hatua ya nane bora ni Dar City yenye pointi 53, UDSM Outsiders (52),Savio (49), Mchenga Star (49), JKT (46), Vijana ‘City Bulls’, (44),  Srelio (42) na ABC (41).

Related Posts