Tofauti kati ya Kongo na Zambia zakaribia kumalizika – DW – 19.09.2024

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na makatibu wakuu wawili wa wizara za biashara wa Kongo na Zambia,madhumuni yake nikukagua utekelezwaji wa makubaliano baina ya serikali za mataifa hayo mawili kuhusu mazingizra  mazuri ya biashara mipakani.

Congo ikiwa kila mara inazitilia shaka shughuli za  Zambia hasa kuhusu uingizaji  bidhaa  Congo, jambo linalopelekea Kinshasa kupoteza pesa nyingi za mapato  ya forodha, wajumbe wa nchi hizo mbili walikagua ghala na vituo vya kuekeshea  magari, kuona ni kipi hasa kinafanyika huko.

Furuaha ya serikali ya Kongo kwa mafanikio mema ya mzozo baina yake na Zambia

Akizungumza na wanahabari baada ya kutembelea ghala na vituo vya kuegeshea  magari, katibu mkuu wa wizara ya biashara ya nchi wa Congo Jules Muilu Mbo alisema amefurahi kujionea kwa macho yake mawili, shughuli zinazofanywa kwenye mipaka, na kwamba mazungumzo ya alhamisi mjini Ndola Zambia, yatasaidia kufafanua zaidi, swala la linalopelekea magari yanayokwenda Kongo kupakulia mizigo kwenye ardhi ya Zambia

Lori likiwa limeegeshwa katika eneo la mpakani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la Kasumbalesa.
Lori likiwa limeegeshwa katika eneo la mpakani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la Kasumbalesa.Picha: Marc JourdierAFP

Zaidi alisema “Tuko hapa kujionea wenyewe kile tunachokisikia na kuona ukweli wa mambo. Na ndio maana tumekuja hapa mahala bidhaa zinapakuliwa. Jeh bidhaa zinapakuliwa hapa kwa njia halali au kimagendo? Jeh, kitendo hicho kinaheshimu kanuni zinazohitajika au lah kwani nchi zetu mbili ni wanachama wa chama wa shirika la biashara ulimwenguni na pia shirika la forodha ulimwenguni.”

Kwa upande wake Lillian Saili Bwalya, katibu wa kudumu wa biashara kwenye wizara ya biashara na viwanda, alijizuiza kuongea, akiahidi kuzingumza, baada ya kikao cha alhamisi mjini Ndola Zambia.

Wasiwasi wa Kongo kwa Zambia na kiini cha tofauti

Kongo ikiwa inashuku Zambia kurahisisha magendo, pale zinapopakuliwa kwenye ardhi yake bidhaa zinazokwenda Congo, makamishna wa forodha upande wa Kongo, wanashuku bei ghali ya malipo ya forodha, jambo linalowapelekea wafanyabiashara wengi kulipa forodha upande wa Zambia, nakuingizaKongobidhaa vyao kupitia njia panya.

Jules Weche, ambae ni mwenyekiti wa chama cha makamishna wa forodha mjini Kasumbalesa alisema “Kongo lazima ishushe bei ya malipo ya forodha, hasa kwa bidhaa vya vyakula. Bidhaa kama bya samaki baridi haviwezilipa dola za kimarekani elfu moja na mia tano Zambia, na Kongo vinalipa dola za kimarekani elfu saba na mia tano.”

Malalamiko ya madereva wa malori

Madereva wa malori yanayochukua mizigo kutoka Tanzania kwenda Kongo, kupitia Zambia, wanalalamikia usumbufu wanaokabiliana nao nchini Kongo, jambo linalowapelekea kupoteza  muda mwingi, na hali hiyo inawasababishia hasara nyingi.

Baadhi ya madereva wakiwa wanayashuku magenge ya vijana kuwavunjia vioo vya magari pamoja nakupasua matairi yao ikiwa hawawapi pesa, wanazoziomba serikali ya Kongo kuboresha usalama. Tukumbushe kuwa, munamo mwezi agosti, Zambia ilifunga mipaka yake na Congo, kupinga hatua ya kupiga marufuku kuingia Kongo kwa bidhaa kama vile Bia, soda na chokaa, iliyochukuliwa na waziri wa biashara ya nje Julien Paluku,agosti iliopita.

Soma zaidi: Watu 37 wahukumiwa kifo kwa jaribio la mapinduzi DRC

Na ni baada ya kumaliza tofauti baina ya Congo na Zambia kuhusu swala hilo, ndio palibuniwa na kamati iliyokutana jumatano na alhamisi hii.

DW Kasumbalesa.

Related Posts