Warioba: Tulipohoji mihimili kuingiliana tulijibiwa ‘tunawashwa washwa’

Dar es Salaam. Jaji mstaafu Joseph Warioba amekumbuka kipindi ambacho alihoji muingiliano wa mihimili ya Bunge, Mahakama na Serikali jambo ambalo amesema halipo sawa kiutendaji, walijibiwa kuwa wanawashwa.

Msingi wa hoja ya Jaji Warioba ilikuwa ni kuonyesha namna mihimili hiyo inavyopaswa kufanya kazi pasi na kuingiliana.

“Nadhani mwaka 2016/17 baadhi yetu tukatoa ushauri kwa wanaoanza kufanya hivyo, ilifikia kiongozi wa Mahakama na Bunge wakawa wanahudhuria vikao vya Rais.

“Viongozi wa mihimili hiyo siyo kama hawakutani bali wanapaswa kukutana kwa njia maalumu mfano kwenye uapisho, lakini katika kazi zao za kawaida hawachanganyiki. Mkiwaleta pamoja watu wataanza kuwa na wasiwasi.

“Na tuliposema tukaambiwa hawa wazee nao wanawashwa washwa. Lakini, si vizuri wakuu hao kukutana kwenye vikao kwani ikitokea wakawa na mawazo tofauti inakuwa na matatizo yake pia,” amesema Warioba.

Warioba ameyasema hayo leo Septemba 19, 2024 jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kilichowakutanisha wadau kujadili tathmini ya hali ya demokrasia nchini.

Related Posts