DC KUBECHA AMALIZA MGOMO WA DALADALA MWAHAKO, MKOANI TANGA

Na Ashrack Miraji (Tanga)

MKUU wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, amemaliza mgomo wa daladala zinazofanya safari kati ya Chalinze, Mwahako, Machaui, na Raskazone. 

Mgomo huo ulisababishwa na barabara mbovu ambazo zimekuwa zikiharibu magari,wanafunzi pamoja wafanyakazi kuchelewa kwenye majukumu yao  hasa wakati wa mvua.

Madereva walitumia fursa hiyo kumuomba Mkuu wa Wilaya kutengenezewa barabara hiyo, ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kutokana na mashimo mengi yanayosababisha kuathiri shughuli za uchumi. 

Wamiliki wa daladala hizo wameeleza kwamba wafanyabiashara wenye mizigo mikubwa wanashindwa kupata huduma ya usafiri kwa kuhofia magari yao kuharibika, pia wanafunzi pamoja na wafanyakazi wanachelewa kufika kwenye majukumu yao hasa vipindi vya mvua.

Mhe. Kubecha aliwahakikishia madereva hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni serikali sikivu na yenye kujali maslahi ya wananchi.

 Alisema kuwa barabara hiyo itakuwa imeshatengenezwa na safari zitaanza tena. Kufikia saa 6 mchana, barabara ilikuwa imebakiza sehemu ndogo ya matengenezo.

DC Kubecha aliwasihi madereva kuwa na uvumilivu na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kwani kufanya hivyo ni ibada na ni kujenga taifa.

Pia, aliwataka madereva kuwa mabalozi wazuri kwa kuwahamasisha vijana kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi bora ambao watakuwa chachu ya maendeleo nchini.


Related Posts