Ngaiza afunika kwa Rebound | Mwanaspoti

FOTIUS Ngaiza wa Vijana ‘City Bulls’, anaongoza kwa kudaka mipira ya ‘rebound’ mara 269 katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD).

Ngaiza aliweza kumwacha kwa mbali mkongwe  Jimmy Brown  wa UDSM Outsiders, anayeshika nafasi ya pili  kwa udakaji mara 203.

Nafasi ya tatu  ilikwenda kwa Elias Nshishi aliyedaka mara 200, Cornelius Ngaiza (Savio) 183, Jordan Jordan  ( Mchenga Star) mara 181.

Wengine ni Amin Mkosa (Mchenga Star) 177, Adam Lutungo (Mgulani JKT) 173, Bramwel Mwombe (Dar City) 160, Robert Tasire (Pazi) 156 na  Isaya Aswile (Chui) 156

Kwa upande wa uzuiaji (Block), aliyeongoza ni; Victor Joseph (Vijana) aliyezuia mara 45, fotius Ngaiza (Vijana ) 41, Jimmy Brown (UDSM) 37.

Wengine ni Jordan Jordan (Mchenga Star), 32, Mchumu (KIUT) 29, Emanuel Chacha (JKT) 28, Bramwel Mwombe (Dar City) 27 na Charly Kesseng (Srelio) 21.

Related Posts