MERIDIANBET YARUDISHA TENA KWA JAMII

Meridianbet leo wameendeleza utamaduni wao wa muda mrefu ambapo wamefika eneo la Mbezi mtaa wa Muafaka jijini Dar-es-salaam na kutoa msaada katika eneo hilo.
Kwa miaka mingi sasa Meridianbet wamekua wakijitahidi kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii ambayo imewazunguka, Leo dodo likiwa limewaangukia wakazi wa Mbezi mtaa wa Muafaka jijini Dar-es-salaam.
Wataalamu hao wa mchezo ya kubashiri wamefika kwenye familia zisizojiweza na kuhakikisha wanatoa mahitaji ambayo yatazigusa familia hizo, Vitu ambavyo vimetolewa ni pamoja na Sukari, Mchele, pamoja na Unga.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka Meridianbet Bi Nancy Ingram alifika eneo la Mbezi kwajili ya kuratibu zoezi hilo na kuhakikisha linakamilika huku akifanikiwa kuzungumza machache “Furaha yangu kuwepo eneo hili leo ni kubwa kwakua tumekuja hapa kuasisi ambayo tumekua tukiyafanya kwa muda mrefu na sio kingine bali kurudisha kwenye jamii yetu haswa kwa wale wenye uhitaji”
Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko sehemu yeyote ile, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.
Wakazi wa eneo la Mbezi Muafaka pia walipata fursa ya kuzungumza baada ya kupokea msaada huo wakishukuru kwa kiwango kikubwa kwa Meridianbet kuwakumbuka kwa kugusa maisha yao, Huku wakitoa wito kwa mabingwa hao wa kubashiri kuendelea na ambacho wanakifanya kwani wanagusa maisha ya Watanzania wengi.

Related Posts