RC Serukamba -Elimu ndio nguzo ya maendeleo ya jamii na uchumi

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amehimiza Wazazi na Walezi Nchini kuhakikisha watoto wao wanapata Elimu na kuwahimiza watoto hao juu ya Umuhimu wa Elimu kwani Elimu ndio Nguzo ya maendeleo ya jamii na Uchumi

Ameyasema hayo leo wakati akihutubia kwenye mahafali ya wanafunzi wa Shule ya Real Hope iliyopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi.

Mhe Serukamba Amesema kuwa jambo kubwa ambalo watoto wanatakiwa kurithi kutoka kwa wazazo wao ni Elimu hivyo wazazi wametakiwa kulipa kipaumbele suala la elimu ili kuleta maendeleo katika jamii

Aidha Mhe. Serukamba ameongeza kwa kuwataka wasomi wote kujijengea tabia ya kujifunza kila siku kwa kusoma vitabu mbalimbali kwani kwa sasa sayansi na teknolojia ikekuwa kwa kasi tofauti na hapo awali.

Vile vile Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mh. Peter Serukamba, ameutaka uongozi wa Shule ya Real Hope pamoja na Kamati ya Shule hiyo kujenga maktaba kubwa ya vitabu kwa ajili ya wanafunzi kujisomea. Amesema kuwa, hivi sasa, wanafunzi wengi wamekuwa wavivu wa kusoma vitabu, hali inayopelekea uwezo mdogo wa fikra.

 

Mh. Serukamba alisisitiza kuwa licha ya juhudi kubwa wanazofanya walimu katika kufundisha na kuwasaidia wanafunzi kufaulu, bado kuna haja ya kujenga maktaba ili kuwapa fursa wanafunzi kujisomea zaidi.

Mkurugenzi wa shule hizo, Bw. Dickson Mwipopo, aliongeza kuwa ni muhimu kwa wazazi kuendeleza mafunzo na maadili mema kwa watoto wao, akisisitiza kwamba mapinduzi dhidi ya ukatili wa kijinsia na matukio mabaya ya uhalifu yatakoma pale wazazi watakapowaelekeza watoto katika misingi ya maadili mazuri waliyopata shuleni.

Related Posts