Tuzo za mwaka huu zitafanyika tarehe 25 Oktoba katika Ukumbi wa Blue Sapphire, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, na tayari zimevutia wadau wakubwa katika sekta ya masoko nchini Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, TMSA imezitumia tuzo hizi kuangazia juhudi na mafanikio ya watu binafsi, mashirika, Taasisi, na wanavyuo wanaofanya mabadiliko katika sekta ya masoko.
Wadhamini wa tuzo za Wanamasoko mwaka huu ni: Fern Marketing, JC Decaux, Hesa Africa, RednWhite, Multchoice Tanzania, Fasthub, Crown Paints, Attwood Marketing, na TCC.
Mkurugenzi wa TMSA Prof. Emmanuel Chao, alielezea namna masoko yalivyo muhimu katika kuhakikisha ukuaji wa chapa na ongezeko la faida. Alisema, “Katika biashara yoyote, masoko ya biashara ni ya kipekee, kwani yanachangia kati ya asilimia 30 na 40 ya bajeti ya biashara, na ni kipengele kikubwa cha kuamua faida na uhai wa biashara.”
“Kama TMSA, tutaendelea kutumia fursa hii kuhamasisha kampuni na wataalamu kuwa na weledi zaidi. Kwa bahati nzuri, tayari tunatoa programu za masoko zenye vyeti. Pia tuko kwenye mazungumzo na Chartered Marketing Institute kutoka Uingereza ili kuoanisha programu zao na zetu. Lengo letu ni kushinda soko la ndani kwa kuzalisha wataalamu wa masoko waliobobea wenye uelewa mkubwa wa soko la Afrika kuliko nje ya nchi,” alimalizia.
TMSA itatoa tuzo kwa washindi katika vipengele kama: Ubora katika Masoko Shirikishi (Interactive marketing/AR & VR), Ubora katika Masoko ya Matukio (Event marketing), Ubora katika Masoko ya Kidijitali (Digital marketing), Ubora katika Masoko ya Uzoefu (Experiential marketing), Kampuni Inayoangazia Jamii ya Mwaka, Timu ya Utafiti wa Masoko ya Mwaka, Mtu wa Masoko wa Mwaka, Ubora katika Uzinduzi/uzinduzi upya wa bidhaa, Nyota inayoibuka ya Mwaka, Kampuni ya Masoko ya Mwaka, Kampuni ya Masoko ya Kidijitali ya Mwaka, Utambuzi wa Umaarufu (Hall of Fame), na Kiongozi Mchanga wa Masoko wa Mwaka.
Washiriki wanaweza kujisajili na kuteua chapa bora kupitia https://tmsa.or.tz au kupitia ChatSoko +255 754 241 241. Baada ya mchakato wa uteuzi, timu ya majaji wenye uzoefu itapitia mapendekezo ya uteuzi na kuchagua washindi wa mwisho.
Mkurugenzi wa TMSA Prof. Emmanuel Chao (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Fern Marketing Caroline Muia (kushoto ), Afisa Masoko wa Fasthub Monalisa Munanka, Afisa Masoko na Mawasiliano wa TMSA Itale Francis, Mkuu wa Mauzo wa Fasthub Christine Abulitsa, na Mkurugenzi Mtendaji wa Fern Marketing Liginiku Millinga (kulia) wakipiga picha wakati wa uzinduzi wa Kongamano na Tuzo za Masoko za TMSA 2024.