UDSM WASHAURI KUWEKWA KWA UZIO SHULE YA MSINGI CHANGANYIKENI

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye,ameiomba halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuweka uzio kwenye shule ya msingi Chakanyikeni iliyopo wilayani humo ili kuongeza umakini kwa wanafunzi waliopo katika shule hiyo.

Amesema hayo leo Septemba 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyoo vya kisasa kwenye shule ya msingi Changanyikeni ambapovyoo hivyo vimejengwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuisaidia jamii.

Amesema changamoto anayoiyona shuleni hapo ni suala la ukosefu uzio.

“Wanafunzi wanahitaji utulivu wakati wa kujifunza hivyo tunaiomba Manispaa kujitahidi kuweka uzio kwenye shule hii ili wanafunzi waweze kujifunza vizuri.”Amesema Prof. Anangisye.

Prof. Anangisye akizungumzia ujenzi wa vyoo shuleni hapo, amesema lengo la chuo hicho ni kuhakikisha elimu nchini inakua kila upande.

Amesema chuo kikuu cha UDSM kinazaidi ya miaka sitini na tatu kimeweza kuinua sekta ya elimu nchini.

Kwa upande wake Afisa Elimu Manispaa ya kinondoni,Mtundi nyamuhangwa,amekipongeza Chuo Kikuu kwa msaada wa ujenzi wa vyoo hivyo na kudai kuwa vitawasaidia kutatua changamoto zilizopo chuoni hapo ya kuwa na matundu machache ya vyoo.

Hata hivyo, Nyamuhangwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amekihaidi chuo hicho kuwa watavitunza vyoo hivyo ili kiendelee kuwa bora.













Related Posts