NA FAUZIA MUSSA
WAZAZI na walezi wametakiwa kushirikiana na walimu wa
madrasa kuwalinda watoto wao na vitendo vya udhalilishaji ambavyo bado vinaonekana kuwepo nchini.
Mbunge wa Jimbo la Chaani, Juma Usonge Hamadi
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu, wazazi na wanafunzi wa madrasat
Nuru-l-huda wakati wa ufunguzi wa madrasa hiyo uiyoambatana
na kusherehekea mazazi ya Mtume Muhammad
S.A.W huko Muharitani Kinyasini Wilayani ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
Alisema licha ya
Serikali na wadau mbalimbali
kukemea vitendo hivyo na adhabu kutolewa
kwa watendaji lakini bado vinaonekana
kujirejea siku hadi siku na kusema kuwa
ipo haja kwa jamii kuimarisha ulinzi
wa watoto ili kuepukana na vitendo hivyo.
“Kutoka na
hali ya utandawazi na mporomoko wa maadili, ni vyema kashirikiana kuwajengea uwezo watoto wetu, wa kujua na kujiepusha na
vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia unaoweza kutokea popote maisha yao hata katika madrasa.” Alisema Usonge
Usonge aliwasisitiza walimu na wazazi kuendelea kuwasimamia watoto kupata elimu zote mbili, na kuwataka wanafunzi hao kusoma
kwa bidii na kuwa na nidhamu kwani ni mambo ya msingi katika kufikia ndoto zao
za maisha.
Mbali na hayo
aliwapongeza walimu wa madrasa hiyo kwa kuwa wastahmilivu kipindi chote walichokuwa
na mazingira magumu ya kufundishia hadi kufanikiwa kupata jengo
hilo litakaloondoa changamoto ya ufinyu wa vyumba vya madrasa iliyokuwepo hapo
awali.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Madrasa hiyo Ustadh
Ali Khamis Foum, alisema suala la udhalilishaji na ukatili wa kijinsia likemewa
katika dini zote, hivyo ni vyema jamiii ikasimamia makatazo hayo ili
kukomesha vitendo vya udhalilishaji
nchini.
Alibainisha
kuwa kupatikana kwa jengo hilo lenye
vyumba vitatu vya kujifunzia, kutaondosha mrundikano wa wanafunzi wengi katika darasa moja, jambo ambalo
alilitaja lingeweza kuhatarisha afya zao.
Vilevile alisema ongezeko la vyumba hivyo pia kutaondoa changamoto ya kuchanganya
wanafunzi wa jinsia mbili katika chumba kimoja, jambo ambalo alilitaja lingechochea
wanafunzi kudhalilishana wao kwa wao
kama halikutatuliwa.
“ Kabla ya jengo hili baadhi ya wanafunzi walilazimika
kusoma nje ya chumba kimoja kilichokuwepo, kupata vyumba hivi itasaidia
wanafunzi wetu wote kusoma ndani” alisema
mwalimu huyo
Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kuwa karibu na
walimu kwani kukose mashirikiano kunazorotesha maendeleo ya elimu kwa
wanafunzi.
Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa madrasa hiyo waliwaomba wadau na wahisani kuwasaidia
kuongeza vyoo katika madrasa hiyo ili kulinda afya za wanafunzi.
“mwanzo madrasa hii ilikuwa na vyoo viwili na
sasa ina vyoo vinne lakini bado havitoshelezi kutokana na wingi wa wanafunzi na
walimu waliopo katika madrasa hii” walisema
Madarasa hiyo ilionzishwa mwaka 1995, ina wanafunzi
257 wakiwemo wanawake158 na wanaume 99,
pamoja na walimu 7 Wanawake 4 na wanaume 3
ambapo katika hafla ya ufunguzi wa madrasa hiyo, mbunge
Usonge alikabidhi kiasi cha
shilingi laki mbili kwaajili ya vikalio na kuahidi kutoa vitabu, vijuzuu
na misahau kwa wanafunzi hao.
MBUNGE wa Jimbo la Chaani, Juma Usonge Hamadi, akikata
utepe kuashiria ufunguzi wa Madrasat Nuru-l-huda iloyopo Muharitani Kinyasini
Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja. (PICHA NA MPIGA PICHA).