Halotel, Ubalozi wa Vietnam Tanzania watembelea kituo cha watoto cha Human Dreams

Na Imani Nathaniel

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Vietnam Tanzania imefanya ziara maalumu katika kituo cha watoto yatima wenye ulemavu cha Human Dreams Children Village na kutoa msaada.

Wafanyakazi wa Halotel wakishirikiana na Ubalozi wa Vietnam Tanzania walifika katika kituo hicho kilichopo Kigamboni na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali, vikiwemo mahitaji muhimu ya kila siku kama vile vyakula, vifaa vya ndani pamoja na fedha.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Halotel, Happy Mushi amesema wanatambua changamoto ambazo watoto wenye ulemavu wanazipitia, ni jukumu lao kama kampuni kuhakikisha kwamba tunawasaidia ili waweze kufikia ndoto zao.

“Tunatumaini msaada wetu utaleta mabadiliko chanya katika maisha ya watoto hawa,” amesema.

Viongozi wa kituo cha Human Dreams Children Village walionyesha furaha yao kwa ziara hiyo, wakisema kwamba msaada wa Halotel na Ubalozi wa Vietnam utawezesha kuboresha hali ya maisha ya watoto wao.

Ziara ya Halotel na Ubalozi wa Vietnam Tanzania imewapa furaha kubwa na faraja watoto hao, ambao mara nyingi wanahitaji upendo na msaada wa karibu kutoka kwa jamii.

Halotel Tanzania inajivunia kuendelea kushiriki katika miradi ya kijamii, kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma bora za mawasiliano na shughuli za kijamii zinazolenga makundi yenye uhitaji.

Related Posts