KUKOSEKANA kwa nyota watatu waliong’ara katika raundi ya tatu ya Lina PG Tour jijini Arusha kunaifanya raundi ya nne ya michuano hiyo inayoanza masaa 96 yajayo mjini Moshi kuwa mbio za farasi wawili kwa upande wa gofu ya ridhaa.
Jay Nathwani alyeshinda raundi ya tatu kwa gofu ya ridhaa na Aliabas Kermali aliyemaliza wa pili na Garv Chadder aliyeshika nafasi ya tatu, wote hawatakuwepo mjini Moshi kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano haya Yasmin Challi.
“Vijana hawa kutoka Arusha hawamo katika orodha ya wachezaji waliojiandiiksha kushiriki michuano ya raundi ya nne licha ya hapo awali kuonyesha nia kushiriki,” alitanabaisha Mkurugenzi wa Lina PG Tour.
Kutokwepo kwa vijana hao kunaofanya raundi ya nne kuiwa ni upinzani kati ya Ally Isanzu wa TPC na Isiaka Daudi Mtubwi wa Dar es Salaam.
Katika michuanoi ya rqauindi yha tatu iliyopigwa katika viwanuja vya Arusha Gymkhana, Isanzu alimaliza katika nafasi ya tano wakati Mtubwi alidshika nafasi ya nne huku nafasi tatu za juu zikishikwa na nyota hao watatu kutoka Arusha.
Raundi ya nne ya Lina PG Tour anaanza rasmi siku Alhamisi katika viwanja vya Moshi Club na jumla ya mashimo 72 yatachezwa katika siku nne za mashindano haya.
Lina PG Tour ambayo ni mashindano ya raundi tano yanayojumuisha viwanja vitano tofauti nchi nzima.
Raundi ya kwanza ilifanyika katika viwanja vya TPC mkoani Kilimanjaro kabla ya viwanja vya Morogoro kuwa mwenyeji wa raundi ya pili mwezi Mei mwaka huu.
Raundi ya tatu ilipigwa Arusha Gymkhana mwezi Julai mwaka huu kabla ya kuipeleka raundi ya nne mjini Moshi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa michuano hiyo raundi ya nne itapigwa mjini Moshi kuanzaia Alhamisi, Septemba 26 hadi Jumapili, Septremba 29 mwaka huu.
Kuelekea raundi ya nne ya mbio za ubingwa wa Lina PG Tour, Ali Isanzu wa TPC ndiye anaongoza licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wachezaji wa Arusha na Dar es Salaam ambao walimpa wakati mgumu katika michuano ya raundi ya tatu jijini Arusha.
Kufuatia matokeo mengine ya raundi za kwanza na pili, tishio kubwa kwa Isanzu ni Isiaka Daudi ambaye ameshika nafasi ya pili nyuma ya Isanzu katika raundi mbil za awali kabla ya kumuacha Isanzu kwa nafasi moja katika raundi ya tatu ya jijini Arusha.
Nuru Mollel haonekani kuwa presha kubwa kwa upande wa gofu ya kulipwa baada ya kuwaacha mbali wapinzani wake wa karibu, Fadhil Nkya na Hassan Kadio wa Dar es Salaam.
Mpaka kufikia mwisho wa raundi ya tatu, Mollel amechukua ushindi katika raundi mbili na kushika nafasi ya pili katika raundi moja.
Mshindi wa jumla wa raundi tano za Lina PG Tour atakata tiketi ya kucheza katika mashindano ya gofu ya dunia katika Falme za Kiarabu na hivyo kuyapa mashindano haya jina la ‘The Road to Dubai’.