Mapokezi ya Hapi Kibiti babu kubwaaa..

Mwenye macho haambiwi tazama! haya ni zaidi ya mahaba na mapenzi kwa chama cha mapinduzi kupitia Jumuiya ya wazazi yanayoineshwa na wanaccm wa Wilaya ya Kibiti mkoani pwani wakimpokea Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM Taifa Ndg. Ally Hapi baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara akiambatana na viongozi mbalimbali yenye lengo la kukijenga chama na kueleza kazi zinazofanywa na serikali uwaletea wananchi maendeleo.

Hapi pamoja na viongozi wa jumuiya hiyo taifa wamepokelewa na mamia ya wananchi wa wilaya ya kibiti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kazi za chama na serikali.

Amewambia kazi kubwa waliyonayo ni kuhakikisha chama cha mapinduzi kinashika dola katika chaguzi zijazo kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na chama hicho.

“Asanteni sana kwa mapokezi makubwa mliyotupa hii Inaonesha namna mnavyokiunga mkono chama cha mapinduzi na mwenyekiti wetu wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan,ninachotaka kuwambia ni kwamba serikali yenu imedhamiria kuwaletea maendeleo na kugusa maisha yenu imeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo bila kujali ni eneo gani hivyo tuendelee kushikamana kwa maendeleo yetu”alisema Hapi

Related Posts