Ninja nje wiki moja, akosa Kombe la Shirikisho

BEKI wa FC Lupopo ya Congo, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema atakuwa nje kwa wiki moja akiukosa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos ya Angola.

Beki huyo wa zamani wa Yanga kwenye mkondo wa kwanza hakuwepo kwenye kikosi hicho kilichopoteza mchezo dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola kwa bao 1-0 kutokana na jeraha la goti.

Akizungumza na Nje ya Bongo, Ninja alisema kwa mujibu wa daktari anaweza kukaa nje ya uwanja kwa wiki moja kisha akarudi kutokana na udogo wa jeraha lake.

Aliongeza, wiki iliyopita alifanya mazoezi ya Gym na sasa anafanya ya uwanjani hivyo atakosa mechi ya marudiano lakini akiziwahi nyingine za ligi.

“Ndiyo nimeanza mazoezi ya uwanjani na daktari kaniambia naweza kurudi uwanjani baada ya wiki moja, hivyo tunaendelea kupambana,” alisema Ninja.

Baada ya kumalizana na michezo ya kimataifa, Lupopo itaanza ligi ikivaana na Makiso Septemba 29 na huenda Ninja akawa sehemu ya kikosi hicho.

Related Posts